Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Happiness akiwa na uso wa furaha pamoja na mama yake,Elitruda

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
 
TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kufanya kipimo cha mwisho kabla ya kumruhusu mtoto Happiness Josephati (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kuwekewa betri kwenye moyo wake.

Akizungumza na matukionamaisha jana hospitalini hapo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano JKCI, Mohamed Maulid alisema madaktari watampima kujua kiwango cha muda ambao betri hiyo itadumu ndani ya muda wake.


“Happiness bado yupo wodini na afya yake imeimarika lakini kabla ya kumruhusu kurudia nyumbani madaktari watamfanyia tena kipimo cha mwisho na kisha watampangia tarehe kurudia tena hospitalini kuchunguza mwenendo wa afya yake,” alisema.


Naye  mama mzazi wa Happiness, Elitruda Malley alisema anamshukuru Mungu kwa maendeleo ya afya aliyonayo mtoto wake huyo hivi sasa baada ya kufanyiwa upasuaji huo.


“Baada ya kufanyiwa upasuaji imebidi tukae kwa muda hadi ijumaa ili kusubiri kipimo hicho, hapa Dar es Salaam sina ndugu hivyo naomba yeyote atakayeguswa aweze kunisaidia,” alisema.


Naye Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi aliyaomba jamii, mashirika na taasisi kujitokeza kusaidia kuchangia matibabu ya wagonjwa wa moyo wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.


“Happiness alisaidiwa na madaktari waliokuja nchini kutoka Marekani kwa kumnunulia kifaa hicho ‘pacemaker’ mama yake hakuwa na uwezo wa kukinunua kwani ni ghali, kuna wengine pia ambao tumeweza kuwafanyia upasuaji kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, ni vyema jamii ikajitokeza kusaidia wagonjwa wengine pia,” alishauri.


Akizungumza hivi karibuni na matukionamaisha katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ambako alilazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, Mtoto huyo alisema anatamani aje kuwa daktari bingwa hapo baadae.

Alipokuwa ICU, akiwa na mama yake na madaktari wake

 "Naendelea vizuri, najisikia nafuu, nashukuru Mungu, nawashukuru wauguzi na madaktari walioweza kunisaidia hadi hivi sasa.

"Nikiwa mkubwa nami natamani niwe daktari bingwa ili niweze kuwasaidia watu wengi dhidi ya magonjwa yanayowasumbua, "alisema Happiness.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement