Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 
Suala la nguvu za kiume linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha baada ya kila siku kuongezeka kwa waganga wanaodai kuwa wanatoa matibabu ya nguvu hizo na kuwawezesha wanaume kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi.

Gazeti la Nipashe limefanya uchunguzi na kugundua kuwa dawa zilizothibitishwa na TFDA ambazo zinaweza kuwasaidia watu wenye matatizo hayo hazizidi tano. Aidha imebainishwa kuwa dawa nyingi zinazotolewa na waganga wa jadi ni hatari kwa afya na huenda zikasababisha matatizo katika mishipa ya damu moyoni.

Afisa Uhusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza alisema kuwa ni kweli kuwa kuna dawa nyingi zinazotangazwa maeneo tofauti nchini lakini miongoni mwa dawa zilizothibitishwa ni pamoja na Viagra, Erecto, Cilais, na Suagra.

Afisa huyo alisema kuwa dawa hizo si za kutumia kiholela kwani mtu anayezitumia lazima awe anauhitaji kweli ama amepungukiwa na ameishiwa kabisa nguvu za kiume. Vinginevyo inaweza kumletea madhara na hata pengine kifo.
 
Dawa hizi tumezipitisha na zimekidhi vigezo vya watumiaji lakini pia zinahitaji watu wanaotakiwa kuzitumia ndio wazitumie vinginevyo zinaweza kuleta matatizo katika mfumo wa damu, alisema Afisa huyo.

Aidha alisema kuwa hawezi kuzungumzia dawa za asili kama vile Mkongoraa, Mkuyati, Vumbi la Kongo ambazo nyingi huuzwa na wamasai kwa madai kuwa zinasaidia kuongeza nguvu za kiume. Aidha alitaka Kitengo cha Tiba Mbadala, Tiba Asili na Wizara ya Afya waulizwe hilo.

Dkt Mkame ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika Wizara ya Afya alisema kuwa sasa wako katika mpango wa kusajili dawa za asili kama zitathibitika kuwa hazina matatizo kwa watumiaji.

 Aidha alisema kwa sasa hakuna dawa yoyote ya asili iliyosajiliwa na wizara ambayo inafaa kutumika na ambayo haina madhara.

Daktari mmoja jijini Dar es Salaam alisema kuwa kikubwa ni watumiaji wa dawa hizo kuwa waangalifu sana wanapotumia dawa hizo hasa zile za asili ambazo hazijathibitishwa kwa sababu zina nguvu sana na ni hatari sana.

Watumiaji wengi wa dawa hio waliohojiwa walisema kuwa walifikia uamuzi wa dawa hizo kwa sababu wapenzi wao hawakuwa wakirizika na tendo la ndoa na hivyo kuwalazimu wao kutumia dawa hizo ili kufanya tendo hilo kwa muda mrefu zaidi.

Source: Nipashe

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement