Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijTki5TtPXCTn5E4RLMC0jGh_Rtsd4CKs-ybV7BoIvKTW6BWVLiygtqFxBgvDZqtmKHkA2DyAq5XXyMTmW2Qw0ZbWAPIw5DMUadAStdlIvnuD3gY8Bue6OuuK8hF2CXFYNq4CP4L70Xzqk/s1600/DSC_0026.jpgNa Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam

MKATABA kati ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Kampuni ya ‘Sunderland Association Football Club’ ya nchini Uingereza ulioidhinishwa mwaka 2013/14, sasa unaitesa bodi hiyo ambayo  inadaiwa Sh. bilioni 3.7.

Deni hilo limetokana na matangazo ambayo kampuni hiyo iliyatangaza kupitia michezo yake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya Wakurugenzi wa TTB, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (Pichani) alisema mkataba huo ni wa hovyo na sasa unaligharimu Taifa.

“Tunadaiwa kwa kuingia mikataba ya hovyo, Mkurugenzi aliyekuwepo wakati ule alikataa kuupitisha matokeo yake akafukuzwa kazi, sijui wengine ilikuwaje wakaupitisha na tunapolipa hili deni nadhani kuna mtu anafaidika nalo hapa nchini.

“Sasa kazi ya Mwenyekiti wa Bodi (Jaji Mstaafu Thomasi Mihayo) ni kututoa hapa tulipo na kuhakikisha kuwa haturudi tena huko. Naiomba bodi hii isije ikakubali kuingia katika mtego wa namna kama hiyo, tumepelekwa mahakamani… tumeshikwa pabaya na lazima tuwalipe sunderland fedha zao,” alisema.

Waziri Maghembe aliitaka bodi hiyo kuhakikisha kuwa inatelekeza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vyote vya utalii vilivyoko nchini ili kuongeza idadi ya watalii.

“Andikeni makala pelekeni kwenye mashirika ya ndege watu watazisoma, msikae ofisini nendeni kule viliko , sekta hii ni kubwa mno kwa sasa inachangia asilimia 17 kwenye pato la Taifa tunahitaji ifike asilimia 30 ifikapo 2018,” alisema.

Aliwataka kutafuta soko la utalii nchini Urusi na kuimarisha lile la Marekani.

“Nendeni Urusi kutafuta soko si kufanya ‘shopping’ warusi wale wana fedha nyingi na sisi tunahitaji fedha. Najua kuna wakurugenzi watatu wa kitengo cha ugavi, utafiti na sheria wameacha kazi kutokana na kwamba mnaidai serikali, tunajua tutashughulikia.

“Lakini naomba mfanye kazi, tuna vivutio vingi ambavyo hatujavitangaza vema matokeo yake Kenya wanatangaza vingine vipo kwao, tusikubali, lazima muongeze idadi ya watalii kutoka milioni moja iliyoko sasa hadi milioni tatu, nitawapima kwa kazi mkishindwa nitawaondoa wote,” alisema.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZ2C58sGyNx830ZK8L_IWbdrQL1lw_3k17e0WmNw_KG4oyCaRLnino779YQzfjef9jn-k1fhpxS8Tw_6QLs7sLuGMIyf4NJuvCLT2bwszbmjhy7cSIORGWtLJ4E1DdaiAnS42wnmWDuKs4/s640/DSC_0097.jpg
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jaji Mstaafu Mihayo (aliyesimama) alimuomba Waziri Maghembe kuisaidia bodi hiyo kwa kulipa madeni ya wafanyakazi yanayotokana na marupurupu yaliyofikia Sh milioni 300.96.

“Viwango vya mishahara havilingani na sekta hii, naomba hilo ulitazame na kutusaidia kulitatua ili watendaji wetu wapate hari ya kufanya kazi na hatutaiangusha serikali,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement