Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kufanya uchunguzi wa kupima magonjwa ya moyo kwa ujauzito unaoanzia wiki 18.

Uchunguzi huo utafanyika hospitalini hapo kwa muda wa siku tatu kuanzia Oktoba 12 hadi 14, mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa JKCI, Maulid Kikondo amesema uchunguzi huo utafanyika bure.

“Tumegundua watoto wengi wanazaliwa na magonjwa ya moyo lakini upo utaalamu ambao wenzetu wamekuwa wakiutumia wa kupima ujauzito ukiwa na wiki 18 na kuendelea ambapo huweza kubaini mapema iwapo mtoto aliyeko tumboni ana matatizo au la.
“Sasa mwenzetu Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto, Naiz Majani alikwenda nje ya nchi na akapata mafunzo, amerudi hivyo tutaanza kuwachunguza wajawazito,” amesema.

Amesema uchunguzi huo utafanywa kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho kitaalamu Fetal Echo-cardiology .

Amesema hawajaweka idadi maalumu ya wajawazito wanaotarajia kuwapima kwa kutumia kifaa hicho na kwamba wanawasihi wafike kwa muda uliopangwa.

“Kila atakayekuja atahudumiwa, mtoto anapogundulika kuwa na tatizo ni rahisi kutibiwa punde tu anapozaliwa na kuwa na afya njema akafurahia maisha kuliko akizaliwa na baadaye kugundulika kwani matibabu yake yanachukua muda ikizingatiwa wengi huletwa wakiwa wamechelewa,” amesema.
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akiwa na Balozi wa China - Tanzania, Dk. Lu Youqing, China ndiyo waliosaidia ujenzi wa JKCI

Kikondo alisema pamoja na hilo, Oktoba 9 hadi 16, mwaka huu wataendesha kambi nyingine ya upasuaji kwa watoto 30 wenye magonjwa hayo.

“Madaktari wa JKCI watafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari wenzao kutoka Addis Ababa wa hospitali ya Al muntada,” amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement