Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
ABE, bodi inayotoa kozi mbalimbali kutoka nchini Uingereza, imeandaa hafla yupi iliyowakutanisha wadau mbalimbali kujadili masuala ya elimu nchini Tanzania na matokeo yake katika ajira kwa vijana.

Hafla hiyo ilishirikisha watu wenye taaluma mbalimbali kama ile watoa elimu, wanafunzi, makampuni ya ajira, maofisa rasilimali watu, wafanyakazi wa makampuni binafsi na serikali, vyombo vya habari na wananchi wengine wanaoguswa na tatizo hilo.
Katika hafla hiyo, jopo lililoteuliwa na waandaaji liliongoza majadiliano yaliyowapa changamoto wadau kutafuta njia za kupunguza tatizo la idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza masomo kila mwaka ambao wanakosa nafasi za ajira.
Majadiliano hayo yalitoa hamasa kwa wadau kubainisha ujuzi na vigezo vinavyohitajika zaidi na waajiri na namna ya kuwasaidia wahitimu kupata ujuzi huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi wa ABE nchini Tanzania, Zaituni Ituja alisema “Wote tunafahamu kuwa wahitimu wengi hawana ajira, lakini pia tunasikia makampuni yanalalamika kuwa hawapati vijana wa kuwaajiri wenye vigezo. Je tatizo ni makampuni hayajui pa kutafuta wafanyakazi au wanapata vijana wasiokidhi vigezo? Swali hili ndio chanzo kikubwa cha sisi kuandaa hafla hii.
Pamoja na majadiliano hayo, wageni walipata muda wa kufahamiana na kubadilishana mawasialiano ya kibiashara kwa lengo la kujenga mahusiano kama ilivyokuwadhamira ya hafla hiyo.
ABE inafanya shughuili zake kwa zaidi ya miaka 40 katika nchi zaidi ya 100 duniani na imewekeza katika kuhakikisha inatoa kiwango cha elimu cha hali ya juu.

Kozi zinazotolewa ni za masomo ya biashara ambazo zinaweza kumsaidia mtu kupata shahada ya chuo au kumuwezesha kupanda cheo. 
ABE inatoa kozi za Business Management, Business Start-up na Enterpreneurship, Human Resouce Management, Marketing Management na Tourism and Hospitality Management.

Kozi hizi zinaweza kusomwa na watu ambao wako kwenye ajira na wanataka tu kukuza uwezo wao na kupanda cheo au wanaotaka kutumia ABE kama njia ya kupata nafasi ya kujiunga na vyuo mbalimbali duniani.

ABE wapo
TPHA Building, plot 66 Victoria, Off Ali Hassan Mwingi Road,
Dar es Salaam, Tanzania

Mawasiliano

Mobile: +255 713 388 758

Website: www.abeuk.com

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement