Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
*Unaweza kuivaa hata mwaka mzima


*Unachopaswa kuzingatia ni usafi pekee
 
*Zinatarajiwa kuzinduliwa Machi, mwaka huu nchini

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MWILI wa binadamu hupitia mabadiliko mbalimbali katika ukuaji wake, kipindi hicho cha mabadiliko ya mwili huitwa balehe, uhusisha mabadiliko yote ya kimwili, kimawazo na kihisia.

Mabadiliko hayo huwapata jinsi zote mbili, ya kike na kiume pale wanapotoka utotoni kuingia utu uzima. Ni katika kipindi cha mabadiliko ya mwili ambapo msichana huanza kupata damu ya hedhi.

Hatua hiyo muhimu uitwa kupevuka(kuvunja ungo), hedhi ni kipindi maalumu katika maisha ya mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa.

Kwa kawaida mzunguko wa hedhi hutokea kila mwezi na kila mwanamke anao mzunguko wake ni hapo ambapo mwili hujiandaa kwa hali ya kupata ujauzito.

Hedhi hutokeaje

Zipo ovari mbili (vifuko vya mayai) katika mwili wa mwanamke, moja upande wa kushoto na nyingine kulia ambazo hutengeneza mayai ya uzazi ambayo husafirishwa hadi katika mji wa mimba kupitia mirija ya uzazi.

Kila mwezi ovari moja huachilia yai mchakato ambao huitwa kitaalamu ovulation na wakati huo mabadiliko ya homoni huuandaa mji wa mimba (uterusi) kutengeneza ukuta mpya uitwao endometrium kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mapokezi ya mimba inayoweza kutungwa.

Yai linalofika katika uterasi iwapo halitarutubishwa na mbegu ya mwanamume, ukuta huo humeguka na kutoka nje ya mji wa mimba kupitia ukeni ukiwa pamoja na damu.

Kitendo hicho ndicho huitwa hedhi (menstruation) au mzunguko wa hedhi (menstruation cycle).
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyVSIgm0gMGl_hgy3kKEpCzRYGzZ4TwotnE2DUQRpAC79NWKyvXSKXRoicx8cNptc8vQQ8ucZs8Zc2o-eBylm97sKqUlieUx4bG_0nYa3Ov4f8CuIN-49oWyClyAYwSD5Zu_NdNlupZpU/s1600/Ciclo-Menstrual.jpg
Inaelezwa kwamba wasichana wengi huanza kupata hedhi yao ya kwanza wakiwa na miaka tisa na kuendelea na mara nyingi mwanamke hukoma hedhi anapotimiza umri wa miaka 45 hadi 50.

Ingawa ni kipindi muhimu katika maisha ya mwanamke lakini huwa kina changamoto ambazo hukumbana nazo na hutofautina kati ya mwanamke mmoja na mwingine.

Wapo ambao hupata hedhi kwa siku tatu na wengine huenda hadi saba na miongoni mwao wapo pia ambao hupata hedhi nyepesi na wengine nzito.

Wapo pia ambao hupata hedhi pasipo kukabiliana na matatizo yoyote lakini wengine hupata hedhi kwa uchungu na masumbufu mengi, kama kuumwa tumbo, mgongo, kichwa, kiuno na mengineyo.

Mwanamke anashauriwa kujiweka safi mwili wake wakati wote hasa akiwa katika kipindi hicho cha kipekee.

Kwa kipindi kirefu wanawake wengi wamekuwa wakitumia njia ya asili hasa mabibi zetu wakitumia vipande vya kanga, vitambaa au vitenge vilivyokatwa kwa ustadi kujihifadhi wakati wa hedhi.

Lakini kukua kwa teknolojia kukapelekea kutengenezwa taulo za kisasa za kutumia na kutupa ambazo huuzwa kwa bei tofauti tofauti madukani.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZaLqmWEYe2qFQ9fj5UWWkt1W-63r3-Dt62C-MjyzRtc-xP5f9YtaCssalLPK-hqKEE4Nm0ZkLqa7MjPcYbnj-PeNmKoPBrPIILfPI6Qt_SKoUpMvkw_JdIi5ua5rDk7LttXAMmXpD154/s400/ms.jpg
Hali ilivyo nchini

Nchini Tanzania suala la hedhi salama hasa kwa wasichana hasa waliopo shuleni linatajwa kuwa bado ni kitendawili na changamoto kwa walio wengi hususan vijijini.

Inaelezwa kuwa wasichana wengi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi hushindwa kuhudhuria masomo yao ipasavyo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano kwa mwezi hiyo.

Hali hiyo inasababishwa na hofu ambayo huwakumba wakiwa katika kipindi hicho, ya kuchafua sare za shule na kuhofia kuchekwa na kutaniwa na wanafunzi wenzao hasa wa kiume walio chini kiumri.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa ikiwemo ile ya haki elimu ya mwaka 2013, kutohudhuria kwao masomo huchangia kuzorotesha kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi husika.

Abuni taulo za kufua

Hali hiyo ndiyo iliyomchochea mjasiriamali Jenipher Shigoli kufanya utafiti akiwa na nia ya kuja na mbinu itakayowasaidia wasichana kutohofia na kuhudhuria masomo yao pasipo kujali kipindi cha hedhi.

“Kitaaluma ni mwanasheria pia ni mwanadiplomasia lakini napenda mno ujasiriamali, nimekuwa nikijihusisha na utengenezaji wa bidhaa za usafi tangu mwaka 2013, kupitia biashara hiyo nimeweza kupata tenda za kusafisha vyoo vya shule mbalimbali nchini kupitia kampeni ya choo salama inayoendeshwa na kampuni ya Malikia ambayo mimi ni Mkurugenzi wake,” anasema.

Anasema kupitia kampeni yake hiyo ameweza kufika katika shule nyingi za mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Iringa.

“Nikiwa katika shughuli hizo za kampeni ya choo salama ndipo nikagundua kwamba wasichana wengi hasa kwa shule za kule vijijini hushindwa kuhudhuria masomo wakiwa katika kipindi cha hedhi kwa hofu ya kuchafuka na kuchekwa,” anasema.


Nini kilimsukuma kubuni taulo hizo

Shigoli anasema alipata nafasi ya kuwahoji baadhi ya wanafunzi ambao walimueleza kuwa ili kujihifadhi hutumia manyoya ya kuku, udongo, magunzi ya mahindi, ugali au soksi.

“Wapo ambao walinieleza huwa wanatumia vitambaa vya kanga au vitenge lakini wataalamu wa afya wanasema si salama kwa afya kwani rangi inayotumika kutengeneza bidhaa hizo kwa kawaida huchuja zinapokuwa zimelowa majimaji.

“Walimu nao walinieleza kuwa wapo wanafunzi wengi ambao huacha masomo na kuamua kukaa nyumbani kwa sababu ya hedhi, kwani hata wale wanaovaa vitambaa huwa hawapo ‘comfortable’ na hali ambayo huwaathiri kisaikolojia,” anasema.

Anasema ni kutokana na adha hizo wanazokabiliana nazo wasichana hasa wa huko vijijini ndizo zilizonifanya nikae chini na kutafuta jinsi ya kuwasaidia.

“Kwa kuwa wengi wanashindwa kumudu gharama za kununua taulo za kutumia na kutupa nilipata wazo la kutengeneza taulo za kutumia zaidi ya mara moja,” anasema.

Alifanikishaje wazo lake

Anasema baada ya kupata wazo hilo aliwashirikisha watu mbalimbali wakiwamo wataalamu wa maabara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shirika la  kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) ambao walimsaidia.

“Walinishauri na tulichukua muda wa miezi sita hadi kukamilisha bidhaa hizo,” anasema.
 
Malighafi ni pamba halisi

Shigoli anasema taulo hizo zimetengezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kwa kutumia pamba halisi, kitambaa na nailoni maalumu ambayo huweza kupokea damu ya hedhi hadi kiwango cha mililita 30 hadi 40.

“Uwezo huo unalingana na ule wa taulo zingine zinazouzwa huko madukani, na huweza kuvaliwa kati ya saa sita hadi saba. Baada ya saa hizo unalazimika kuifua na kuianika ikauke vizuri kwa ajili ya kuitumia tena na hudumu hadi mwaka mmoja,” anasema.

Atunukiwa tuzo

Anasema kupitia bidhaa yake hiyo aliweza kuibuka mshindi katika shindano la kusaka wabunifu barani Afrika mwaka jana linalosimamiwa na taasisi ya ‘African Entrepreneur  Award’.

“Niliibuka mshindi wa kwanza na nilizawadiwa kiasi cha Dola 150,000 sawa na Shilingi milioni 300 za Kitanzania,” anasema.

Serikali yampa eneo la kiwanda, mtaji

Jenipher anasema anaishukuru serikali kupitia Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kwani imenipatia mtaji wa Sh milioni 30 ili kukuza biashara yake hiyo.

“Kupitia Wizara hiyo nimepewa eneo la kutosha kujenga kiwanda huko Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizi tunatarajia kukizindua ifikapo Machi, mwaka huu,” anasema.

Anasema tayari pia ameshapeleka barua Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwamba anatarajia atapata ushirikiano wa kutosha aisaidie jamii yake.
Jenipher anawasihi watanzania hasa wanawake kutokuwa na wasiwasi juu ya taulo hizo alizobuni.

“Nimepitia taratibu zote kisheria, zimepimwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zimeonekana zina ubora, nimeenda pia Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) nimepewa ‘certificate’ na kama nilivyoeleza awali kuna wataalamu ambao nashirikiana nao kutoka UDSM na SIDO,” anasema.
 http://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/12E7/production/_91193840_c1e5a719-41a0-4db3-bf5b-2f7a45451090.jpg
Mbegu za uzazi za mwanaume zikikimbilia kwenye yai kutengeneza mtoto

Simulizi ya Monica

Monica Elius (si jina lake halisi) anasema ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu aanza kutumia taulo hizo za kufua na kwamba amebaini tofauti kubwa ikilinganishwa na zile za kutumia na kutupa.

“Sikujua kama kuna mbunifu Mtanzania ambaye ameanza kuzitengeneza pia taulo za aina hii nchini, maana nilianza kuzitumia muda mrefu sasa umepita na nilikuwa najua kwamba zinatoka nje na kuletwa kama msaada.

“Nina dada yangu ambaye mume wake alikuwa akifanya kazi katika kambi ya wakimbizi iliyopo Ngara mkoani Kigoma, wanawake na wasichana waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo walikuwa wakigawiwa na mashirika ya misaada,” anasema.

Alianzaje kuzitumia

“Awali nilikuwa natumia taulo za kawaida zinazouzwa madukani, lakini kila nilipotumia nilikuwa napata muwasho mkali mno, hali yangu ilikuwa mbaya,” anasema.

Anasema alikuwa analazimika kwenda hospitalini kupima na kupewa matibabu kila mara ingawa haikugundulika tatizo lilikuwa nini hadi anapatwa na hali ya namna hiyo.

“Nakumbuka kuna wakati nilikuwa mkoani Morogoro nilitokewa na hali hiyo nikaenda katika dispensary moja na kumuelezea daktari niliyemkuta, alinipima na kugundua kuwa nina mzio na hizi taulo za kawaida.

“Hivyo alinishauri ninunue kanga mpya nikate vipande vya kunitosha au ninunue gozi (kitambaa maalumu ambacho hutumika kufunga vidonda) pamoja na pamba ili nijitengenezee taulo zangu mwenyewe,” anasema.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZaLqmWEYe2qFQ9fj5UWWkt1W-63r3-Dt62C-MjyzRtc-xP5f9YtaCssalLPK-hqKEE4Nm0ZkLqa7MjPcYbnj-PeNmKoPBrPIILfPI6Qt_SKoUpMvkw_JdIi5ua5rDk7LttXAMmXpD154/s400/ms.jpgWasichana wengi hupata maumivu ya tumbo wakiwa katika siku za hedhi

Gozi ni gharama kubwa

Anaongeza “Hata hivyo nilishindwa kumudu hilo kwani nilikuwa natumia fedha nyingi kununua gozi peke yake ni kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000 na pamba ni kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000 kwa hiyo nilihitaji kati ya shilingi 60,000 hadi 70,000 niweze kupata bidhaa hizo ili nitengeneze taulo za kutumia miezi mitatu hadi minne, ni gharama kubwa mno.

Anasema siku moja akiwa na dada yake huyo alimshangaa kuona anahangaika kutengeneza vitambaa vya kujihifadhi jambo ambalo lilimlazimu kumsimulia sababu za kufanya hivyo.

“Alinishangaa, ikabidi nimsimulie ndipo akaniambia atanipatia hizo taulo za kufua, sikuamini kama zipo hadi siku aliponiletea,” anasema.

Anasema taulo hizo huuzwa kati ya Sh. 5,000 hadi 8,000 na kwamba tangu ameanza kuzitumia ameondokana na ile hadha ya kupatwa muwasho katika sehemu zake za siri.

“Unaona kama hii niliyobeba (akimuonesha mwandishi wa makala haya) ina mwaka sasa lakini bado naitumia, haijachoka kama unavyoiona,” anasema.

Uzoefu wake

Monica anasema taulo hizo zimetengezwa na malighafi ya pamba pekee na kitambaa maalumu hali ambayo inaifanya kuwa laini na murua wakati wote anapokuwa ameivaa.

“Yaani ni laini kiasi kwamba unajisikia raha ukiwa umeivaa hakuna michubuko wala huwezi kujihisi harufu mbaya unapokuwa umeitumia, hata ukipata muwasho si kama ule unaotokea ukiwa umevaa taulo zile za kutumia na kutupa,” anasema.

Anasema hiyo ni kwa sababu taulo hizo hazijatengenezwa na kemikali yoyote zaidi ya pamba na kitambaa hicho maalumu.

Anaongeza “Kwa kawaida huwa zinakaa taulo nne katika pakiti moja, mbili huwa ni nzito kwa ajili ya kutumia katika kipindi ambacho damu ya hedhi huwa nyingi na nyingine mbili ni nyepesi kwa ajili ya kutumia katika kipindi wakati hedhi ikiwa si nyingi.
 http://i.ytimg.com/vi/tGrHHUXshMQ/maxresdefault.jpg
Zinafuliwaje?

Anasema suala la usafi wa taulo hiyo ni wa muhimu kuuzingatia ili mtumiaji asipate matatizo mbalimbali ya kiafya kama vile muwasho na hata harufu mbaya.

“Huwa nafualia sabuni ya unga, naona ndiyo inafaa zaidi kuliko zingine. Hii unapaswa kuifua na kuisuuza vizuri kwa maji mengi, ukisuuza na maji kidogo ikikauka unaikuta ina alama za mistari zimekatisha katikati,” anasema.

Anaongeza “Alama hizo hufanya muonekano wake kuwa wa kuudhi, uzuri ni kwamba unapoifua na kuianika kukiwa na jua kali haichukui zaidi ya saa mbili unaikuta tayari imekauka na unaweza kuivaa tena.

Anaongeza “Nampongeza huyo mbunifu Mtanzania kwa kuliona na kulifanyia kazi wazo hilo, ni taulo nzuri hata ukiwa safarini, wanawake tukiwa safarini na kupatwa na hali hiyo kama sehemu uliyopo hakuna maji huwa ni shida kubwa.

“Lakini ukiwa safarini na ukawa umetumia taulo hii ni tofauti na zile za kutupa, ukijisafisha hubaki na harufu, unahifadhi vizuri taulo yako na kwenda kuisafisha nyumbani pindi unapofika,” anasema.

Anasema taulo hizo zinasaidia kupunguza gharama kwani mtu anaponunua huweza kukaa nazo hadi mwaka mzima.

“Naona ni mkombozi hasa kwa wenzetu walioko vijijini ambako tunajua ni kazi mtu kupata shilingi 2,000 au 3,000 ya kununua pakiti ya taulo za kawaida.

“Akinunua hii kwa shilingi 5,000 au 8,000 anakuwa na kazi ya kuzingatia ufuaji safi na anazitumia mwaka mzima, lakini kupanga ni kuchagua, kila mmoja ana maamuzi yake, binafsi nazipenda, ninapoivaa najisikia huru na mchangamfu wakati wote nikiwa kwenye siku zangu,” anasema.
 https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/11/Acute-Abdomen.jpg
Daktari 

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), (jina linahifadhiwa kwa sasa anasema kipindi cha hedhi ni muhimu kwa afya ya mwanamke.

“Mwanamke anapokuwa katika siku zake hulazimika kutumia taulo hizo ambazo kazi yake kuu ni kupokea ile damu inayotoka, kama hatavaa maana yake ni kwamba itapitiliza kuchagua nguo zake.

“Taulo za kutumia na kutupa jinsi zilivyotengenezwa zina ‘layer’ maalumu kwa ndani ambayo hufyonza damu ya hedhi, hulazimu kubadili mara nyingi (kiasi cha kila baada ya saa nne) hasa inapokuwa inatoka kwa wingi,” anasema.

Kauli ya TBS

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Egid Mubofu anasema ni kweli shirika hilo lilipokea maombi ya kupima taulo hizo za Elea hata hivyo bidhaa hiyo bado haijaruhusiwa kuingizwa sokoni.

“TBS tulipokea maombi kutoka kampuni ya Malkia ambao ni wazalishaji wa bidhaa za Elea. Upimaji wa awali wa bidhaa hiyo ulifanyika na matokeo yalionesha kuwa bidhaa hiyo haikidhi kiwango cha bidhaa husika ambacho ni TZS 1659:2014, hivyo mzalishaji akatakiwa  kufanyia marekebisho bidhaa hiyo,” anasema.

Mubofu anasema mpaka sasa mzalishaji wa bidhaa hiyo hajafanyia marekebisho bidhaa hiyo, hivyoTBS bado haijathibitisha ubora wa bidhaa hiyo.

Bidhaa za pedi ziko katika orodha ya bidhaa za lazima, hii ni kutokana na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza endapo bidhaa hizo hazitakidhi matakwa ya kiwango husika. Hivyo basi bidhaa za aina hii hazipaswi kuingizwa sokoni mpaka hapo ubora wake utakapothibishwa,” anasisitiza.

Kauli ya Shigoli

Mbunifu wa taulo hizo, Shigoli anasema bidhaa yake hiyo bado hajaiingiza sokoni kuanza kuwauzia wateja.
Anasema kwa sababu anaboresha eneo lake la kiwanda kama ambavyo ametakiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
 
“Bado sijaingiza sokoni bidhaa ya Elea, kwa sababu TBS wamenitaka nihakikishe naboresha kwanza eneo langu la kiwanda, hivi sasa najenga kiwanda huko Kibaha mkoani Pwani ambapo eneo nimepewa na serikali,” anasema.

Anasema baada ya kukamilisha kiwanda chake hicho maofisa wa TBS watakwenda tena kumkagua kujiridhisha kabla ya kumpa kibali cha kuweka nembo ya ubora katika bidhaa yake hiyo.

“Natarajia ujenzi wa kiwanda utakamilika ifikapo Machi, mwaka huu na tutazindua bidhaa yetu rasmi, nitakapopewa ruhusa ya kuweka nembo ya ubora na itaanza kupatikana sokoni,” anasema.
 http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2016/12/Pg-33.jpg

Kauli ya Wizara 

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni EATV hivi karibuni, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (pichani) alisema serikali inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kuna uwezekano wa kupata taulo za hedhi (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.


“Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuangalia zile pedi ambazo vijana wanaweza kutumia mwenzi mmoja, miwili hata mwaka mzima, hata kwa miaka miwili. tunaendelea kuangalia tafiti mbalimbali kuhusu usalama wa hizi pedi ambazo zinaweza kuzitumia kwa muda mrefu,” alisema.

Aliongeza, “Kwa hiyo tunaangalia kama na sisi tunaweza kuziruhusu kuingia nchini na sisi tuziingize sokoni. Lengo letu ni kuangalia usalama kwanza kabla hatujaziruhusu kutumika.

Alisema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa yakuambukizwa.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement