Ijumaa, 24 Februari 2017

ANWANI MPYA YA WIZARA YA AFYA, BAADA YA KUHAMIA DODOMA. SOMA HAPA.

Image may contain: 3 people, outdoorJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inapenda kuufahamisha Umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Mkoani Dodoma imetekelezwa tarehe 23 Februari, 2017.


Image may contain: one or more people and outdoor Miongoni mwa waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Mhe. Dk. Hamis Kigwangalla.
Image may contain: one or more people, sky, cloud and outdoorWengine ni Makatibu Wakuu wa Wizara Idara kuu ya Afya na Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Image may contain: sky, cloud and outdoor Kufuatia Uhamisho huo, jumla ya watumishi 90 wa Wizara hiyo wameungana na viongozi wao kuitikia uhamisho huo.

Image may contain: one or more people, shoes and outdoor Anwani za Wizara zitakazotumika mkoani Dodoma ni kama ifuatavyo:

Katibu Mkuu,
 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

Idara Kuu ya Afya,


Chuo Kikuu Dodoma,


Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,


S.L.P 743,


Jengo Namba 11, 


DODOMA.


Namba ya Simu +255 26 2323267

 Image may contain: outdoor
Anwani nyingine 

Katibu Mkuu,
 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
 

Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
 

Chuo Kikuu Dodoma,
 

Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,
 

S.L.P 573,
 

Jengo Namba 11
 

DODOMA.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO
24/2/2017