Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

https://i.ytimg.com/vi/IcCzgaL-MRY/hqdefault.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

VIJANA wengi nchini bado hawawezi kuandika wasifu wao  wanapofikia hatua ya kutafuta ajira na hivyo kujikuta wakiisha kunakili wasifu wa watu wengine hasa zilizowekwa mtandaoni hatua ambayo imeelezwa kuwa haifai.

Aidha, vijana ambao huhitaji kujiajiri nao hushindwa kutengeneza wazo zuri, kulifanya liwe bora na jinsi gani wanaweza kutumia fursa za kibenki zilizopo kupata mikopo kuendelea mawazo yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sostenes Kewe alisema hayo jana alipozungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa mafunzo ya ujasiriamali na ajira kwa vijana kwa njia ya mtandao uitwao Noa Ubongo.

“Vijana wana ndoto za kupata maendeleo lakini wengi hujikuta ndoto zao hazitimii kutokana na sababu mbalimbali, kwa mfano wale wanaotaka kutafuta ajira tumegundua hawajui kuandika wasifu wao matokeo yake wananakili za watu wengine na kukosa kazi.

“Wanaotaka kujiajiri nao hawajui kutengeneza na kuliboresha wazo la biashara, sasa kupitia mpango huu wa Noa Ubongo watapata elimu hii kupitia njia ya mtandao,” alisema.

Kewe alisema utafiti kuhusu Elimu ya Mambo ya Fedha wa mwaka 2014 unaonesha asilimia 58 ya watanzania hawajibidiishi katika kutafuta taarifa mbalimbali kwa kujisukuma wenyewe.

Alisema utafiti huo unaonesha pia asilimia 68 hawana ule uthubutu wa kutafuta elimu ya mambo ya fedha na hivyo kushindwa kuchangamkia fursa nyingi zilizopo huko.

“Kwa hiyo huu ni wakati mwafaka kwa vijana na watanzania kwa ujumla kufuatilia vipindi vya Noa Ubongo ili waweze kupata elimu ya kibiashara ambayo itawasaidia kutoka kimaisha,”  alisema.

Naye Nisha Sanghvi wa Khanga Rue Media, alisema wameamua kutumia njia ya mtandao kwani ni rahisi kuwapata vijana wengi kuwafikishia ujumbe huo walionao.

“Noa Ubongo ni chaneliya kwa ajili ya vijana ambayo inawafundisha ujuzi utakaowasaidia kuongeza uwezo wao, kubadili mtazamo wao na itakayowasaidia kuboresh kifedha maisha yao ya baadae,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement