Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

*KUZAA MFULULIZO HUCHANGIA MAMA KUPATA MTOTO NJITI


NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

KUZAA watoto wengi ni mojawapo ya desturi zilikuwapo katika jamii nyingi za kiafrika, enzi za mababu zetu familia iliyokuwa na watoto wengi ilipewa heshima ya kipekee katika jamii.

Familia iliyopata idadi kubwa ya watoto ilijiona kuwa bora kuliko zingine na hapo baba mwenye familia husika alijiona kuwa ni shujaa.

Pamoja na kuwa jitihada nyingi zimefanyika kuelimisha jamii umuhimu wa kupanga uzazi, wapo walioipokea elimu hiyo lakini pia bado wapo wachache ambao wanaendelea kutekeleza desturi ile ya kuzaa watoto wengi.

Pengine ulikuwa hujui kwamba, wataalamu wanasema mama anayejifungua watoto wengi yupo kwenye hatari ya kuzaa mtoto kabla ya kutimiza muda wake halali wa miezi tisa?
 http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3054086/medRes/1242002/-/dk64px/-/kinachosababisha..jpg
Watoto wanaozaliwa kabla ya muda unaokusudiwa mara nyingi huwa na uzito pungufu, wengi wetu tunawaita watoto hawa ‘njiti’.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Wachanga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Augustino Masawe anasema ingawa bado haijajulikana wazi sababu zinazosababisha mama kuzaa mtoto njiti.
Lakini, tafiti zikiwa zinaendelea kufanyika, kitendo cha mama kuzaa mfululizo kinatajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayotajwa kuchochea mama kuzaa mtoto njiti.

“Idadi ya watoto njiti inazidi kuongezeka kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, hapa Muhimbili kwa mfano tangu kuanzishwa kwa kitengo cha kulea watoto hawa kati ya miaka ya 1990 tulikuwa tukilaza watoto 30 lakini leo hii idadi imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 1000.
 http://dar24.com/wp-content/uploads/2016/05/KITETE.2.jpg
Mashine ya kusaidia watoto wanaozaliwa njiti

“Zipo sababu nyingi zinazochangia ongezeko hili ikiwamo mama kuzaa mfululizo. Unajua afya ya mama ni ya muhimu mno kuizingatia tena tangu akiwa tumboni kwa mama yake, akizaliwa, na hadi anapokuja kushika mimba.

“Lakini tatizo linakuja kwamba huyu mama mimba yake ililelelewa kwa shida, na yeye kutokana na umasikini anakuja kubeba mimba na anailea kwa shida na wengi ni katika umri mdogo halafu unakuta mwingine anazaa pasipo kupumzika, hili ni tatizo,” anasema.

Anasema mama anayejifungua watoto mfululizo bila kujipa muda wa kupumzika mlango wake wa kizazi huwa katika hatari ya kufungua wakati wowote ikilinganishwa na mama anayezaa kwa kupumzika na kuacha kipindi fulani cha muda kupita.

“Jambo lingine ambalo tunaona linapaswa kufanyiwa kazi ni ujenzi wa afya ya mama. Nchini Tanzania tunaona kina mama wengi wanaojifungua hii leo ni watoto kwa maana ya kwamba wanajifungua chini ya umri wa miaka 18 unaoshauriwa kitaalamu.

“Hawa ni karibu asilimia 20, mara nyingi hawa huzaa watoto njiti kwa sababu viungo vyao huwa havijakomaa kuweza kuhimili ile hali ndiyo maana inashauriwa familia ziwaache watoto wakue kwanza,” anasema.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqAgXKQZdICCQ5_P7kuV5tKmSbf12Feywe6-ENd4JqHlQvqXGA171Qz1NxqSqNbTdCipyiQeqtkNhPLB24khmi5CplMPtrc-6F7lqlmDwtay8FNDxYVdDxrjyPj3m1MIdBCFAHWnVolauE/s640/05.JPG
Daktari huyo anasema wa mama wengine hujikuta wakizaa watoto njiti au hupoteza mimba zao kabisa kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo upungufu wa damu, malaria za mara kwa mara, shinikizo la damu na magonjwa mengine.

“Pamoja na hayo maisha duni tunaweza kutaja kuwa husababisha wengi kuingia katika tatizo zaidi kuliko wale wanaoishi maisha yenye unafuu. Kwa mfano hapa Dar es Salaam unaweza kuona hali hiyo zaidi katika maeneo ya Mbagala au Tandare lakini si maeneo kama Oysterbay.

“Mama mwenye mimba ya pacha naye huwa kwenye uwezekano wa kuzaa mtoto mmoja akiwa njiti, ndiyo maana tunashauri sana sana jamii izingatie mno kujenga afya ya mama kwani ni muhimu ili aweze kupata mtoto aliye na afya bora katika maisha yake,” anasema.
 
Tafiti

Tatizo la watoto kuzaliwa wakiwa na uzito pungufu (njiti) ulimwenguni linalizi kuongezeka kadri miaka inavyosonga mbele hasa katika ukanda wa Jangwa la Sahara, ikiwamo Tanzania.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kati ya watoto 10 wanaozaliwa ulimwenguni, mmoja huzaliwa akiwa na uzito pungufu.

Wataalamu wa afya wanasema mtoto anayezaliwa na uzito pungufu hupambana na madhara mengi katika ukuaji wake.
Kwamba tatizo hilo huathiri moja kwa moja ukuaji wake na hivyo kushindwa kuishi kwa afya kama ilivyo kwa watoto wengine waliozaliwa na uzito unaoshauriwa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0TvjsH9FOsoethbVrS_Zvhasy_YKOM5gj6aLa0YdvdJa9PWXCY1xytEITPPijBjRvZT7SathO47bw8zyFbaE1gfWyGVRt6rKsFhyaKfKeONFxlxOSwRd3ugN30flaNCyy4hm27jBePJk/s1600/8Waziri+Ummy+Mwalimu+Akimpakata+Mtoto+Mchanga+Katika+Wodi+Mpya+Iliyozinduliwa.jpg
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifurahia jambo na mmoja wa wazazi aliyejifungua salama hivi karibuni.

Hali ilivyo Muhimbili

Takwimu za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), zinaonesha idadi hiyo imeongezeka maradufu kutoka watoto 30 mwaka 2012 hadi kufikia watoto 1,500 mwaka 2015/16.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dk. Julieth Magandi hiyo inamaanisha kuwa kuna ongezeko la watoto njiti 1,200 katika kipindi cha miaka minne pekee.

Huchangia vifo vya watoto.

Dk. Magandi anasema kwa mujibu wa takwimu za WHO wastani watoto milioni 15 huzaliwa njiti ulimwenguni kote kila mwaka.

“Inakadiriwa hapa nchini, asilimia 13 ya watoto huzaliwa wakiwa na uzito pungufu na huchangia kwa takriban asilimia 86 ya vifo vya watoto wachanga,” anasema.

Anasema kwa kuwa mtoto anapozaliwa njiti huwa ni rahisi kupata madhara mengi hivyo huhitaji kupatiwa uangalizi wa hali ya juu.

“Iwapo atapewa uangalizi wa karibu huwa ni rahisi kupoteza maisha , huhitaji kupata joto la kumsaidia kukua na kwa kuwa mapafu yake hayana uwezo mzuri wa kupumua huhitaji msaada wa ziada.
 http://www.mamaye.or.tz/sites/default/files/evidence/Kangaroo%20care_2.jpg
Mama akiwa amembeba mtoto kwa njia ya kangaroo

Uzito pungufu wa kuzaliwa una madhara makubwa na huathiri ukuaji wa watoto wachanga kuishi na kukua,” anasema.
Daktari huyo anaongeza “Asilimia 27 ya vifo vya watoto hao husababishwa na magonjwa yatokanayo na vimelea vya bacteria na matatizo ya upumuaji.

“Tunatumia njia ya kangaroo ambapo mama humfunga kifuani pake na kukaa naye, hivi karibuni tumeweza kupata dawa ya kukomaza mapafu lakini ni ghali, dozi kwa ajili ya mtoto mmoja ni milioni 1.2,” alisema.

“Wale wanaozaa pacha nao mara nyingi hutokea wakapata mtoto njiti, lakini pia asilimia 20 ya wanaojifungua siku hizi nchini ni watoto yaani wapo chini ya umri wa miaka 18 unaoshauriwa, hawa wapo katika hatari ya kuzaa watoto njiti,” alisema.
 http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/11/TOT1.jpg

Jitihada zinazofanyika 

Dk Magandi (katikati juu) anasema hatua ya Muhimbili kuanzisha kitengo cha Kangaroo imesaidia kuokoa maisha ya watoto wengi waliozaliwa wakiwa njiti.

“Katika muongo mmoja uliopita Tanzania ilikuwa kati ya nchi zilizoweza kufikia lengo namba nne la Mpango wa Malengo ya Milenia la kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga.

“Muhimbili kupitia mpango wa Kangaroo tumeweza kupungua vifo vya watoto hawa, wengi wanapona kwa kiwango cha asilimia 90 sasa,” anasema.

Anasema kwa kutumia njia ya kangaroo mtoto huweza kupata joto analohitaji moja kwa moja kutoka katika mwili wa mama yake.“Lakini pia afya ya mwanawe ikibadilika ghafla na hata akishindwa kunyonya au akipaliwa na maziwa huwa ni rahisi pia kugundua, kwa njia hii mama anakuwa muuguzi mkuu, hivyo akiona mtoto anapata shida anaomba msaada wa haraka wa daktari,” anasema.http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/09/ujauzito.jpg?resize=595%2C401

“Njia ya kangaroo husaidia mtoto kupata joto zuri, mama hulazimika kumfunga kifuani kwake, kwa hiyo huwa rahisi kwake kufuatilia kwa karibu mwenendo wa afya ya mwanawe.

“Lakini pia afya ya mwanawe ikibadilika ghafla na hata akishindwa kunyonya au akipaliwa na maziwa huwa ni rahisi pia kugundua, kwa njia hii mama anakuwa muuguzi mkuu, hivyo akiona mtoto anapata shida anaomba msaada wa haraka wa daktari,” anasema.

“Lakini pia afya ya mwanawe ikibadilika ghafla na hata akishindwa kunyonya au akipaliwa na maziwa huwa ni rahisi pia kugundua, kwa njia hii mama anakuwa muuguzi mkuu, hivyo akiona mtoto anapata shida anaomba msaada wa haraka wa daktari,” anasema.

 Makala haya kwa mara ya kwanza yalichapishwa Desemba, mwaka jana katika gazeti la MTANZANIA, kisha ikachapishwa katika mtandao huu Desemba12, mwaka jana.
Veronica ni mwandishi wa gazeti la MTANZANIA na mwendeshaji wa Blog ya matukionamaisha


Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement