Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiv1Ojf8oZIhSLJ0-DM7y6HRBRqL09Mb9pJc5DktGqb0zkdTQwKzx_lOInA9f-s_e1hTo21iJ5ex4AwjbN6tbHLC6ppEeuvwtju-M8wq1xZyn45CCD6DUsQ5IEks7L9H4xI2Bv2JnYXDqc/s1600/ngao.png 
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangalla amesema watu wanaohusika na ukusanyaji wa taarifa za kihistoria watakwenda kumfanyia mahojiano Francis Maige (86).

Dk. Kingwangalla alisema hayo juzi wakati alipokwenda kumjulia hali Maige ambaye maarufu kwa jina la Ngosha ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa (bibi na bwana) katika Hospitali ya Amana ambako alikuwa amelazwa kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

“Inawezekana kuna vitu vingi bado hatuvijui kuhusu nembo hii, watakuja watu wa kukusanya historia kumuhoji mzee Maige naamini kuna mambo mengi atawaeleza,” alisema.
 Picha ya Catherine Sungura
Dk. Kingwangalla akimjulia hali Mzee Maige

Akizungumza, Mzee huyo alisema nembo hiyo aliibuni na kuichora mnamo mwaka 1957 pamoja na mwezake Ali Panga mwenyeji wa Tanga ambaye hata hivyo kwa sasa ni marehemu.

“Tulichora nembo hiyo mwaka 1957 baada ya kupewa tenda, tuliambiwa kwamba itatumika pindi Mwenyezi Mungu atakapotujalia kupata uhuru na kweli tulipata,” alisema.

Pamoja na hayo, Ngosha alisema anampango wa kumpatia Rais John Magufuli zawadi ya picha tatu ambazo amezichora.

“Ninazo picha tatu, ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na ya kwake mwenyewe (Rais Magufuli ambazo nimepanga kumpatia zawadi,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement