Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akielezea jambo wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Bunge la Uganda waliotembelea Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wametembelea Taasisi hiyo ili kujionea namna inavyofanya majukumu yake
NA VERONICA ROMWALD – DAR – ES SALAAM
Kamisheni ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda kuvutiwa
na mafanikio ya utoaji huduma za kutibu magonjwa ya moyo zinazotolewa katika Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Kamisheni hiyo jana ilifanya ziara ya kujifunza katika
Taasisi hiyo mapema asubuhi ikiongozwa na Kamishna wake, Ceclia Barbara.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishina huyo alisema
JKCI imepiga hatua kubwa na kutoa huduma bora kwa watanzania hali ambayo
imesaidia kupunguza idadi ya rufaa za wagonjwa wa moyo kwenda nje.
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakifuatilia Maelezo kuhusu
namna JKCI inavyofanya kazi wakati
wa ziara yao katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
“Uganda tunatoa huduma za tiba ya moyo ingawa tuna
changamoto nyingi zinaikabili sekta ya afya, lakini wenzetu wameyapata kwa muda
mfupi wa takriban miaka mitatu wamesaidia watanzania wengi,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo maana waliona vema kufanya
ziara hiyo ya kujifunza.
“Sisi kama wanasiasa tumejifunza vitu vingi hapa kwa
mfano tumeona uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali hapa, na kuanzia sasa
mnaweza kuona wataalamu wetu wengi wakija kujifunza,” alisema.
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakiwa katika sehemu ya mapokezi
ya kuingia Wodi ya Watoto.
Aliongeza “Lakini pia tumetoa ombi letu kwa uongozi wa
JKCI ili tushirikiane nao watusaidie wataalamu wake waje nchini mwetu ili kutoa
mafunzo haya.
alisema ipo haja kwa nchi zilizopo kwenye jumuiya ya
Afrika Mashariki kushirikiana kwa dhati na kujifunza miongoni mwao ili kusaidia
wananchi wengi zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI
Profesa. Mohamed Janabi akipeana mkono na Kiongozi wa Msafara wa baadhi
ya Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara wakati wa ziara yao katika
Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza.
“Niliwahi kufika Tanzania mara kadhaa, na kila
ninapokuja naona mabadiliko makubwa hasa katika sekta ya afya, naipongeza
serikali ya Tanzania kwa uwekezaji uliofanyika katika sekta ya afya… kuja kwetu hapa leo
(jana) tumehamasika mno,” alisema.
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akizungumza
alisema wamepokea ombi la Kamisheni hiyo kwamba wapo tayari kuwapa mafunzo.
“Tutakwenda kuwapa mawazo ili nao wapige hatua, takwimu zinaonesha Uganda kwa miaka mitano
wamehudumia wagonjwa 850 JKCI imeweza kuhudumia wagonjwa 1000 kwa kipindi cha
mwaka 2016/17.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mussa Zungu akizungumza jambo mbele ya Wabunge kutoka Uganda
walipotembelea JKCI. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka
Uganda Mhe. Cecilia Barbara na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa. Mohamed Janabi (katikati).
“Kipindi cha mwaka 2014 tuliona wagonjwa 5000 lakini
mwaka huu hadi sasa tumeona wagonjwa 40,000, tayari tumewafanyia upasuaji wa
bila kufungua kifua kutibu magonjwa ya moyo wagonjwa 620 na wagonjwa 150
tumewatibu kwa njia ya kufungua kifua,” alisema.
Aliongeza “Leo (jana) tumefanya upasuaji mkubwa wa
kuweka benti kubwa kwenye moyo iitwayo kitaalamu CRTD na tunatarajia kuwafanyia
wagonjwa 20 upasuaji huo ambao ikiwa wangeenda India ingegharimu Sh milioni 120
kwa kila mgonjwa mmoja lakini hapa JKCI wanagharimu Sh milioni 35 hadi 40
pekee.
Alisema changamoto inayowakabili sasa ni ufinyu wa
nafasi ambapo wana jumla ya vitanda 128 kwa ajili ya watoto na watu wazima.
“Lakini hili linafanyiwa kazi na serikali, iwapo
tutapata nafasi kubwa nchi itapiga hatua zaidi,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge la Tanzania,
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu alisema kwa kuwa wajumbe wa kamisheni
hiyo wamekuja kutizama masuala ya afya nchini walipendekeza kuwafikisha kujifunza
JKCI.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI)Profesa. Mohamed Janabi (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es
Salaam
“wamefurahi mno na wameona jinsi ambavyo Tanzania
tumeweza kupunguza idadi ya wagonjwa tunaowapa rufaa kwenda India kutoka 300
hadi wanne mwaka jana, ni kutokana na uwekezaji huu tuliofanywa,” alisema.
Alisema ili kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa
katika taasisi hiyo serikali imepatia fedha zote za maendeleo (OC) ambazo
waliziomba.
Chapisha Maoni