Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

https://s-media-cache-ak0.pinimg.com/736x/3c/84/48/3c84489791e61fba400045c69457ce64--crazy-eyes-visual-development.jpgNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

Macho ya mtoto wako yanapobadilika na kupata kengeza jambo unalotakiwa kufanya ni kumuwahisha hospitalini afanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu sahihi.

Makengeza yametajwa kuwa ni miongoni mwa dalili za saratani ya jicho ambayo inaonekana kuwatesa watoto wengi katika miaka ya hivi karibuni.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Judith Mwende alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na MTANZANIA kwenye mahoajiano maalumu.

Mahojiano hayo yalijikita kuzungumzia tatizo la saratani ya jicho kwa watoto, ambapo alisema kila mwaka wanapokea watoto kati ya 100 hadi 150 wanaougua ugonjwa huo.

“Asilimia 70 hadi 90 ya watoto tunaowapokea wanaletwa wakati ugonjwa ukiwa upo katika hatua za tatu na nne, katika hatua hizi ugonjwa unakuwa umesambaa kwa sehemu kubwa,” alisema.

Dk. Mwende alisema wazazi wengi wanapohojiwa wanaeleza kwamba waliona mabadiliko mbalimbali katika macho ya watoto wao lakini walidhani ni ya kawaida.

“Wapo ambao wanatueleza walianza kuona macho yamepata kengeza, ingawa si mara zote, lakini mara nyingi kengeza ni miongoni mwa dalili za saratani ya jicho kwa watoto,” alisema.

Daktari huyo alitaja dalili zingine za awali za tatizo hilo ni weupe kwenye mboni ya jicho, jicho kuvilia damu, jicho kuwa jekundu na kupata maumivu.

“Dalili nyingine ni mtoto wa jicho, jicho kuwaka kama paka usiku au mwanga mweupe pindi unapopiga picha na ‘flash’ na dalili zingine hutokea kadiri ugonjwa unavyozidi kukomaa kwa mfano jicho kuvimba na kuwa kubwa,” alisema.

Aliongeza “Hivyo ni vema wazazi wanapoona mabadiliko haya na mengineyo wasipuuze na kukaa nao nyumbani wakiwatibu wenyewe kwa kununulia dawa bila ushauri wa daktari, wawalete hospitalini wapate tiba stahiki.

“Ingawa dawa zote ni halali kwa matumizi na salama lakini ni hatari hasa zinapotumika bila kufuata maelekezo maalumu ya wataalamu wa afya, zinaweza kusababisha upofu,” alifafanua.

Habari hii imetoka leo kwenye gazeti la MTANZANIA leo

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement