Jumanne, 11 Julai 2017

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, Framan Swai akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Otilia Guelo na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA-Tanzania), Dkt. Hashina Begum walipotembelea banda la Ingenderhealth lililokuwa likitoa huduma za uzazi wa mpango viwanjani hapo leo.

 Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
 
WAKAZI wa Temeke leo wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mwembe Yanga wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani ambapo wamepatiwa elimu kuhusu masuala ya uzazi wa mpango.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Otilia Guelo na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA-Tanzania), Dkt. Hashina Begum walipotembelea banda la Tanzania Youth Vision and Coalition (TYVC).

Wakipatiwa maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

 Huduma zilizotolewa uwanjani hapo ni pamoja na ushauri nasaha kuhusu maambukizi ya VVU na UKIMWI pamoja na upimaji afya, huduma za uzazi wa mpango pamoja na elimu kuhusu njia mbalimbali za uzazi wa mpango.

Wakiwa katika banda la Maria Stopes.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema ipo haja kwa watanzania kuzingatia elimu wanayopewa juu ya uzazi wa mpango ili kudhibiti kasi ya ongezeko la kuzaliana nchini. 


Wakiwa katika banda la Chama cha Uzazi na Malezi Tanzania (UMATI).

Amesema mmonyoko wa maadili katika jamii nao umechangia ongezeko la watu kuzaliana hivyo vijana wanapaswa kupatiwa elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi, ili wajitambue na kujiepusha na kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo.


Naye Dk. Begum amesema iwapo jamii itapatiwa elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi wa mpango itasaidia kukabili ongezeko lililopo.

Amesema hali hiyo itasaidia serikali kuokoa kiasi cha Dola moja hadi sita ilizowekeza kwenye mpango huo ambazo zitakwenda kusaidia kukuza uchumi katika shughuli zingine za kimaendeleo.
Ofisa Habari wa UNFPA, Wallen Bright akimfafanulia jambo mwanahabari Ally wakati wa maadhimisho hayo.

Picha zote na Veronica Romwald.