Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

http://wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/802400852.jpgNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Mfumo wa Chakula wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Tuzo Lyuu ameleza adhara ambayo mtu huweza kupata kutokana na kunywa kinywaji hicho.

Akizungumza na mtandao huu, Dk. Lyuu amesema kwa kawaida sprit ambayo watu huitumia kutengeneza kinywaji hicho huwa imebeba ndani yake sumu iitwayo kitaalamu methanol.

Dk. Lyuu amesema sumu hiyo huwa haihitajiki kabisa ndani ya mwili wa binadamu na kwamba pindi inapoingia mwili hushindwa kuihimili.

“Mchanganyiko wanaoweka hutengeneza vitu vingi ambavyo vina madhara makubwa kwa mwili wa binadamu zaidi kuliko pombe za kawaida ambazo tunazijua,” amesema.

Ameongeza “Ni kwamba katika utengenezaji wa hicho kinywaji tunajua huwa kuna 'temperature' tofauti za utengenezaji na kukusanya zile 'product' (zinazochanganywa).

“Kwa hiyo ukikusanya zile product katika temperature ya tofauti unaweza kupata mchanganyiko mkubwa wa ile alcohol pamoja na hiyo methanol.

“Wakati kinywaji hicho kinapotengenezwa, 'correction' ya kwanza inayotoka huwa ni hiyo methanol ambayo ikichanganywa na alcohol hupatikana hiyo sumu ambayo haihitajiki kabisa mwilini,” amefafanua.

Amesema sumu hiyo ina madhara makubwa katika mwili wa binadamu kwani huenda kuathiri moja kwa moja baadhi ya viungo hasa macho na ubongo.

“Yaani sumu hiyo ya methanol pindi tu inapoingia mwilini, mwili hushindwa kabisa kuzihimili na matokeo yake husababisha kifo kwa muhusika,” amesisitiza.

Dk. Lyuu amesema iwapo mjamzito atatumia kinywaji kilichotengenezwa kwa namna hiyo huenda kumuathiri pia mtoto aliyembeba tumboni mwake.

“Kwa hiyo ina madhara makubwa kwa watumiaji wote,” amebainisha.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement