Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akimjulia hali mmoja
wa wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)
MIAKA
MIWILI YA MH. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI - SEKTA YA AFYA YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA.
TUNAKUPONGEZA KWA KUWEKEZA KWENYE AFYA NA USTAWI ZA WATANZANIA
Katika kipindi cha miaka miwili
ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe
Magufuli,Serikali kupiti Wizara ya Afya imeleta maboresho makubwa ili
kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. Tunajivunia mambo makuu 6.
HALI
YA UPATIKANAJI WA DAWA YAZIDI KUIMARIKA
Hali ya
upatikanaji wa dawa inaendelea kuimeimarika ambapo hadi Oktoba 2017, asilimia
80 ya dawa muhimu (Essential Medicine)135
zinazohitajika katika vituo vya kutolea
huduma za afya vya Serikali nchini zinapatikana kwenye maghala ya
Bohari ya Dawa (MSD) ikilinganishwa na
36% iliyokuwepo mwezi Juni 2015.
Hili imefanikiwa kutokana na uamuzi wa Mhe Rais Dr John Magufuli wa kuongeza
fedha kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa Dawa, Vifaa, na Vifaa Tiba, pamoja
na Chanjo kutoka shilingi Bilioni 31 mwaka 2015/2016 mpaka Shilingi Bilioni 251.5 mwaka 2016/2017 na
kufikia shilingi Bilioni 269 kwa mwaka 2017/2018.
Bei ya
dawa muhimu zaidi imepungua kwa wastani wa asilimia 30 kutokana na uamuzi wa
Serikali kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Mfano dawa ya kupambana na maambukizi ya backteria (amoxicillin/Clavulanic
Acid Potassium 625mg) yenye vidonge 15 awali ilikuwa inauzwa na MSD kwa
shilingi 9,800/=, kuanzia Julai 2017 inauzwa shilingi 4,000/=.
HUDUMA
ZA MATIBABU YA KIBINGWA ZAIMARIKA NA HIVYO KUPUNGUA KWA WAGONJWA WANAOPELEKWA
NJE YA NCHI KWA AJILI YA MATIBABU
· Huduma
za Matibabu ya kibingwa zimeimarishwa na hivyo kuwezesha huduma hizi kupatikana
kwa wananchi wengi na kwa gharama nafuu.
Hatua hii pia imewezesha kupungua kwa Idadi ya wagonjwa waliopelekwa nje ya nchi kwa gharama za Serikali kutoka
wagonjwa 423 mwaka 2015 na hadi
kufikia wagonjwa 203 mwezi Oktoba 2017.
Mafanikio haya ni kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanywa katika
Hospitali za Kitaifa za Serikali.
Hospitali
za Taifa Muhimbili (MNH)
· Serikali
imeiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufanya maboresho mbalimbali
ikiwa ni pamoja na;-
-
Ununuzi wa Vifaa Tiba vya Kisasa kama CT-Scan
iliyofungwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
-
Kuongeza Vitanda vya Wagonjwa Mahututi (ICU)
kutoka 21 mwaka 2015 na kufikia 74 mwaka 2016/2017
-
Kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 mwaka
2015 na kufikia 20 mwaka 2017 na hivyo kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri
kutoka miaka 2 hadi miezi 4 au 6 .
-
Kujenga Vyumba 2 vya upasuaji kwa watoto ambapo
sasa upasuaji unafanywa kwa watoto 50 kwa wiki kutoka watoto 15 kwa wiki mwaka
2015 na hivyo kupunguza muda wa watoto kusubiri upasuaji kutoka miaka 2 hadi
miezi 4.
-
Mashine kwa ajili ya kusafisha damu kwa wagonjwa
wa figo (dialysis) zimeongezeka kutoka 27 mwaka 2015 hadi kufikia 42 na hivyo
kupunguza muda na mrundikano wa wagonjwa wanaohitaji huduma za kusafisha damu
nchini
-
Kuanzisha Huduma za kupandikiza vifaa vya
kuongeza usikivu (Cochlear implant) na hivyo kuwezesha watoto waliozaliwa na
matatizo ya usikivu kupata huduma hizi kwa gharama ya shilingi milioni 34 kwa
mtoto badala ya shilingi milioni 80 iwapo wangepelekwa kupata huduma hii nje ya
nchi. Vilevile MNH iko mbioni kuanza huduma za upandikizaji figo kabla ya
mwisho wa mwezi Desemba 2017.
Madaktari
bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu katika Taasisi ya Jakaya Kikwete
(JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji
UPASUAJI
WA MOYO
· Huduma
za Upasuaji wa Moyo nchini kupitia Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) zimeboreshwa. Hivi sasa JKCI ina uwezo wa
kupasua wagonjwa 3 kwa siku sawa na
wagonjwa 90 kwa mwezi ikilinganishwa na kupasua mgonjwa 1 kwa siku ,sawa na wagonjwa 15 kwa mwezi tangu kuanzishwa
Taasisi hiyo mwaka 2016. Hivyo fedha
nyingi ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi zimeokolewa na ujuzi wa
Wataalam wetu umezidi kuimarika. Aidha JKCI imeanza kupokea wagonjwa kwa ajili
ya upasuaji wa moyo kutoka nchi jirani ikiwemo Malawi,Kenya, Burundi, Uganda, Comoro,
DRC, Rwanda na Zambia.
MATIBABU
YA SARATANI
· Kuhusu
matibabu ya Saratani Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Serikali
imeongeza vitanda na vifaa vya kuwahudumia wagonjwa wanaopata tiba ya saratani
kwa njia ya dawa (Chemotherapy) kutoka wagonjwa 40 mwaka 2015 hadi 100 mwaka
2017. Taasisi imepunguza muda wa wagonjwa kusubiri kuanza tiba ya Mionzi
(Radiotherapy) kutoka miezi 3 hadi wiki 6. Muda huo utaendelea kupungua hadi
kufikia wiki 2.
Upatikanaji wa dawa za
saratani umeboreshwa kutoka asilimia 4 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia
80 mwezi Oktoba 2017, na kwa baadhi ya saratani kama ya mlango wa kizazi,
saratani ya koo na tezi dume dawa za dripu (chemotherapy) zinapatikana kwa
asilimia 100.
KUONGEZEKA
KWA WANANCHI WALIOJIUNGA NA MIFUKO YA BIMA YA AFYA
· Kupitia
azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za
afya bila kikwazo cha fedha, hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kuhamasisha
wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya kuugua. Hatua
hii imewezesha kuongezeka kwa idadi ya
Watanzania waliojiunga na Mifuko ya Bima ya Afya kutoka 27% mwaka 2015/16 hadi
31.5% Septemba 2017 sawa na wananchi wapatao 15,675,396.
HUDUMA
ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO ZABORESHWA ZAIDI
·
Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto zimeboreshwa
ambapo Serikali inanunua, kusambaza na kutoa
bila malipo dawa kwa ajili ya uzazi salama kwa wanawake wote wajawazito wanaofika katika vituo vya kutolea
huduma vya Serikali ikiwemo dawa kwa
ajili ya kuongeza damu (Fefol), dawa ya kuzuia
kutokwa na damu baada ya kujifungua (Oxytocin),
pamoja na dawa kwa ajili ya kifafa cha mimba (Magnesium Sulphate). Pia, Serikali imegawa magari ya kubebea
wagonjwa (Ambulance) 67 aina ya Land Cruiser katika Halmashauri za Mikoa yote
ya Kanda ya Ziwa na Kigoma na Mikoa mingine hapa nchini ili kuimarisha huduma
za rufaa kwa wagonjwa hasa wanawake wajawazito.
· Ili
kuokoa maisha ya mama na mtoto mchanga, Serikali ya awamu ya tano inaanzisha
ujenzi wa miundombinu muhimu kwa ajili ya kutoa huduma za uzazi za dharura
ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni ambapo vyumba vya upasuaji (Theatres) vipatavyo 170 vinajengwa
katika Vituo mbalimbali vya Afya nchini. Kukamilika kwa mpango huu kutaongeza
idadi ya vituo vya Afya vya Serikali (Health Centres) vinavyotoa Huduma za
uzazi za Dharura ikiwemo upasuaji kutoka 109 ya mwaka 2016 na kufikia 279 mwaka
2017 na hivyo kuokoa maisha ya mama na mtoto mchanga.
KUPANUA
WIGO WA UPATIKANAJI WA DAWA ZA ARV NA MATIBABU YA KIFUA KIKUU
·
Kuanzia mwezi Oktoba 2016, Serikali imeanza
kutoa dawa za ARV kwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya VVU/UKIMWI (WAVIU)
bila kujali kiwango cha CD4 ambapo hadi kufikia Oktoba 2017, jumla ya WAVIU
wanaotumia ARV/ART ni 935,228
zilizokuwa zikitolewa katika vituo vya huduma za tiba na matunzo vipatavyo
6,259 nchi nzima. Idadi hii ni sawa na
asilimia 67 tu ya watu 1,400,000 wanaokadiriwa kuwa na maambukizi ya VVU
nchini.
·
kuanzia Desemba 2016, Serikali imeimarisha na
kusogeza huduma za uchunguzi na matibabu ya kifua kikuu sugu karibu na wananchi
kutoka Hospitali moja ya
Kibongoto (Kilimanjaro) mwaka 2015 hadi Vituo 18 vilivyoko katika mikoa 9 ya
Geita, Dar es salaam, Mtwara, Morogoro, Pwani, Mbeya, Kagera, Tanga na Simiyu
VITANDA
VYA WAGONJWA NA MASHUKA VYASAMBAZWA NCHI NZIMA
Ili
kutimiza ahadi ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kila kituo cha
kutolea huduma za afya cha Umma kinakuwa na vifaa vya kutosha, Serikali
imenunua na kusambaza kwa kila Halmashauri vitanda vya Hospitali 20, vitanda
vya kujifungulia 5, magodoro 25 na mashuka 50. Jumla ya vitanda vya Hospitali
vya kawaida (Hospital beds) 3,680, vitanda vya kujifungulia (delivery beds)
920, magodoro 4,600 na mashuka 9,200 vimenunuliwa na kusambazwa.
Waziri,Naibu
Waziri,Menejimenti pamoja na Watumishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto tunashukuru na kukupongeza Rais wetu Mpendwa kwa
Juhudi zako za dhati katika kuboresha huduma za Sekta ya afya nchini
“Tutaendelea
kutekeleza”
Chapisha Maoni