Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo wa MOI wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa kuondoa uvimbe chini ya fuvu la kichwa.

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mgongo, Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) inazidi kuimarisha huduma zake za upasuaji mkubwa na mdogo.

Awamu hii madaktari bingwa (wazalendo) wa upasuaji ubongo na mgongo wa taasisi hiyo, wamefanikisha upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe uliokuwa chini ya fuvu la kichwa kwa njia ya kisasa.
Umakini mkubwa huhitajika kukamilisha upasuaji wa aina hii ambao huchukua hata saa nne kukamilika.

Daktari Hamisi Shabani amesema wameuondoa uvimbe huo kwa njia ya upasuaji wa matundu madogo kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho endoscopic.

“Tumemfanyia mtoto ambaye alizaliwa na tatizo la kichwa kikubwa, aliwahi kufanyiwa upasuaji na kuwekewa mrija maalum kutibu tatizo hilo.

“Ikaonekana baada ya kuwekewa mrija huo alipata shida nyingine, ikabidi tumfanyie tena upasuaji, tumeutoa na tumezibua baadhi ya mishipa iliyokuwa imeziba na tumeondoa uvimbe uliokuwa umejitokeza kwa njia ya upasuaji wa matundu,” amesema.

Amesema huo ni muendelezo wa matibabu ambayo yameanza kutolewa Desemba 16, mwaka huu ambapo watoto wapatao 30 wamefanyiwa kutibu tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Nasra Idi ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam amewashukuru madaktari wa taasisi hiyo kumfanyia upasuaji mtoto wake aliyekuwa na tatizo la kichwa kikubwa.

Naye, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo wa MOI, Laurent Mchome alisema wamemfanyia upasuaji wa kuondoa uvimbe chini ya kichwa ambao ulimsababishia mgonjwa kupoteza uwezo wa kuona.

Meneja Uhusiano na Ustawi wa MOI, Almas Jumaa amesema upasuaji wa aiana hiyo umeanza hivi karibuni katika taasisi hiyo.

Baba huyu mtoto wake ana tatizo la mgongo wazi anasema ana imani kwamba Mwenyezi Mungu atawajalia madaktari hao kufanikisha upasuaji wa mtoto wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye watoto waliozaliwa na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi (ASBHAT), Abdulhakim Bayakub ametoa rai kwa wazazi kuwawahisha hospitalini watoto wenye matatizo hayo na si kuwaficha majumbani.

"Tunaomba pia wadau waendelee kujitokeza kutusaidia kupata vipandikizi maalum (shunts) ambazo madaktari huzitumia kupandikiza ili kusaidia kuondoa maji yanayokuwa yanajaa katika kichwa cha mtoto," amesema.

Picha zote na Veronica Romwald

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement