Jumapili, 17 Desemba 2017

PATEL SAMAJ BROTHER- HOOD WAFADHILI MATIBABU YA WATOTO 10 JKCI


Mwenyekiti wa Ukoo huo, Harish Patel amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi 

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WATOTO 10 wanaosubiri matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), wamelipiwa gharama za matibabu na Ukoo wa Patel Samaj kiasi cha Sh milioni 22.5.
Mwenyekiti wa Ukoo huo, Harish Patel amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi mapema leo hundi ya kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza amesema imekuwa utamaduni wao wa muda mrefu kusaidia jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Janabi amewashukuru wana ukoo hao kwa msaada wa fedha hizo.

Wamepata nafasi pia kuwatembelea watoto waliolazwa wodini.

Wana-ukoo hao wamegawa pia zawadi mbalimbali kuwafariji wagonjwa waliopo wodini ikiwamo matunda na vinywaji.

Patel Samaj Brother-Hood na wanachama wa Baps Charity wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi.

Picha zote na Veronica Romwald