Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
IMG-20180116-WA0052
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri matibabu katika Kituo cha Afya cha Mbozi Mkoani Songwe katikA.

Na WAMJWW-SONGWE.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Momba iliyopo Mkoani Songwe Mh. Said Ilando kumchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumtoa katika nafasi hiyo, kutokana na matumizi mabovu ya pesa zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa Thieta, Wodi ya kujifungulia, Chumba cha mama na Mtoto, Maabara, Mochwari na Nyumba ya watumishi.

IMG-20180116-WA0053 Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya cha Mbozi Mkoani Songwe.

 Amebainisha hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Songwe katika Halmashauri yamji wa Tunduma ya Kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa katika vituo vya Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kushiriki shughuli za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa vituo vya Afya.

Dkt. Ndugulile alisema kwamba Mkandarasi huyo hafai kuendelea na ujenzi wa kituo hicho kwasababu ya kutokidhi viwango vya ubora na kufanya urasimu katika fedha ya umma kwa kuitumia vibaya huku majengo aliyojenga kukosa ubora.

“Mnafanya mchezo na fedha za Serikali, tutawafunga nawaambia, Pesa tulizotoa ni kwaajili ya ujenzi wa Thieta, Wodi ya kujifungulia, Chumba cha mama na Mtoto, Maabara, Mochwari na Nyumba ya watumishi tu, nyie mnaenda kujengea ukuta, nawaambieni tutawafunga” alisema Dkt. Ndugulile kwa jazba sana.
IMG-20180116-WA0054
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akizungumza na moja ya mgonjwa alipotembelea kituo cha Afya cha Mbozi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Mkoani Songwe ya kukagua huduma za Afya katika vituo vya Afya 

 Mkandarasi huyo anaefahamika kwa jina la Sospeter Lutonja amekwisha tumia Zaidi ya Milioni 100 kukarabati nyumba ya mtumishi, ilioonekana kuwa na kasoro nyingi licha ya kumalizika na kujenga msingi wa thieta nao ukionekana kuwa na kasoro nyingi huku akishindwa kutumia ramani katika ujenzi wa majengo hayo.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kumwandalia taarifa ya mipango ya matumizi ya pesa hiyo ambayo ni Milioni 500, na kuwaonya wakishindwa kufanya hivyo atazichukua pesa hizo na uzielekeza katika Halmashauri nyingine zenye uhitaji wa pesa hiyo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Momba Mh. Said Ilando alikiri kuwepo kwa kosa hilo na aliahidi kumchukulia hatua Mkandarasi huyo kwa matumizi mabovu ya pesa hizo, lakini pia kwa kushindwa kusimamia vizuri ujenzi huo licha ya kupata semina ya matumizi ya pesa mazuri kupitia akaunti inayohusisha jamii katika shughuli za ujenzi wa vituo hivyo  yaani Forced akaunti. 

Mh. Said aliendelea kusema kuwa kamati ya ujenzi ya kituo cha Afya cha Tunduma kwenda katika Halmashauri  nyingine ambazo zinafanya vizuri katika ujenzi wa majengo hayo kwa gharama ndogo inayotokana na kutumia Forced akaunti.
IMG-20180116-WA0055
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua kifaa aina ya microscope.  

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya Wakati anawasilisha taarifa yake alisema kuwa kiwango cha matumizi ya njia mbali mbali za uzazi wa mpango ni asilimia 45 ukilinganisha  na asilimia 44.6 huku kiwango cha kitaifa kikiwa Asilimia 27,  huku changamoto ikiwa ni wajawazito kuchelewa kuanza kliniki mapema.

Kwa upande mwingine Dkt. Kheri Kagya alisema kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kupitia huduma ya ushauri nasaha (VCT) ni asilimia 4 ambapo kitaifa kwa utafiti wa mwaka 2016/2017 (THIS) maambukizi ya UKIMWI ni asilimia 5.8 kwa Mkoa wa Songwe, aidha huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 40,988 wlipimwa VVU kati yao 1,616 (3%) walikutwa na maambukizi ya VVU.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement