Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile akikagua jokofu la kuhifadhia chanjo alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za afya mkoani Rukwa.

Na WAMJWW. RUKWA-NKASI

Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

“Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri, Dk. Ndungulile akipata maelekezo ya ramani ya jengo jipya la mama na mtoto katika kituo cha Afya Nkolomo kutoka kwa wataalamu.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.

“Dawa zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ” aliendelea Dkt. Ndugulile.

Ziara ikiendelea

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta, Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya wananchi (fixed akaunti). 

Akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.

Dkt. Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223 vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.

Kwa upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement