Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akisisitiza jambo katika kikao hicho

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAFANYAKAZI wapya 57 walioajiriwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi ametoa rai hiyo leo alipozungumza katika kikao kazi kati yake na wafanyakazi hao.

"Hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayekiuka kanuni na maadili ya kazi, jiepusheni na vitendo vya rushwa na zingatieni majukumu yenu mtakayopangiwa pamoja na kuvaa mavazi ya staha hasa kwa wale ambao watakuwa hawavai 'uniform'," ametoa rai.

Kikao kikiendelea

Wafanyakazi hao wakimsikiliza kwa makini Profesa Janabi wakati alipokuwa akizungumza nao.

Picha zote na Veronica Romwald

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement