Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Dk. Respicious Boniface (aliyesimama pichani) ameihakikishia Bodi ya wadhamini ya taasisi hiyo kwamba wataendelea kufanya kazi kwa weledi mwaka 2018.

Amesisitiza watafanya hivyo ili kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora kwa wakati muafaka.

Dk. Boniface alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao kati ya wafanyakazi, viongozi waandamizi wa MOI na wajumbe wa bodi hiyo. 
Awali akizungumza wakati akitoa salamu za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Zakia Meghji (Pichani) aliwapongeza wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwahudumia watanzania waliopata matatizo mbalimbali hasa kutokana na magonjwa ya ajali.

Alisema anatambua kazi kubwa na ngumu wanayofanya madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania wanaofikishwa katika taasisi hiyo.

“Natambua kazi kubwa inayofanyika hapa usiku na mchana ili kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wanaotokana na ongezeko la ajali hapa nchini,” alisema. 
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.

Aliongeza “Sisi kama Bodi tunatambua kazi kubwa na nzito mnayofanya, kwa waliopo nje ya MOI si rahisi kutambua hilo. Nawapongezeni sana, na niwatie moyo kwamba tutashirikiana ili kupambana na changamoto zinazojitokeza.

Alisema ana imani kwamba kazi kubwa zilizofanyika mwaka 2017 zitaendelea na kuboreshwa zaidi katika mwaka 2018 ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora hapa hapa nchini. 
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.

Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa, vifaa tiba na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wagonjwa na watoa huduma.

“Sasa hivi hakuna msongamano wodini au wagonjwa kulala chini kwa kukosa vitanda,” alisema. 
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Bakari Lembariti aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kuendelea kutimiza dira ya MOI kuwa Kituo cha Weledi Afrika na kuendeleza ubunifu katika utoaji huduma ambazo hazifanyiki katika nchi nyingi za kiafrika.

“Hatua hiyo imeifanya MOI kuwa Kituo cha Weledi Afrika katika tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, mnastahili pongezi,” alisema.

Mjumbe wa Bodi hiyo, Dk. Eric Aris alisema watakwenda kuzishughulikia changamoto zote walizoelezwa na wafanyakazi hao ili kuhakikisha kwamba utoaji huduma bora huathiriki kwa njia yoyote ile.
Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.


Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.



Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha Uhusiano na Ustawi wa Jamii MOI

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement