Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
Serikali inakusudia kuanza kununua dawa za kuhifadhia maiti moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji viwandani.
Hatua hiyo itachukuliwa ili kusaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa gharama ya kuhifadhi maiti katika hospitali mbalimbali.
Kauli
hiyo ilitolewa Dar es Salaam le na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake aliyofanya katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa ya Amana.
Katika
Hospitali hiyo wananchi hulipia kiasi cha Sh 30, 000 kwa siku ikiwa ni
gharama za kuhifadhiwa miili ya ndugu na jamaa zao waliofariki dunia.
"Changamoto
hii ipo katika maeneo mengi nchini, hivyo tunakusudia kuanza kununua
dawa hizi moja kwa moja kwa wazalishaji na kisha tutatoa bei elekezi kwa
ajili ya kumpunguzia gharama mwananchi," amesema.
Awali alisema anaridhishwa na utendaji kazi hospitalini hapo.
Chapisha Maoni