Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri Ummy akiwa katika wodi ambayo wagonjwa wamehamishwa ya Mwaisela.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na utekelezaji wa agizo la kuhamisha wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwenda Hospitali ya Tiba na Taaluma Mloganzila (MAMC).

Hayo ameyasema wakati alipotembelea MNHi kuangalia hali ya utoaji wa huduma pamoja na utekelezaji wa agizo hilo alilolitoa wakati alipotembelea Hospitali ya Tiba na taaluma Mloganzila mapema mwezi huu.

“Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa waliopo kwenye jingo la Mwaisela kuaznia wodi namaba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa wagonjwa mahututi na wenye kesi maalumu ila nawapongeza wametekeleza agizo hilo mara moja” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewapongeza MNH kwa  kuwahamisha madaktari bingwa 15 na wauguzi zaidi ya 30 kwenda katika Hospitali ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma sawa na inayotolewa Muhimbili.

Alisema utekelezaji wa agizo hilo umewezesha kupatikana nafasi na kuiagiza Muhimbili kuwapatia nafasi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili waweze kuongeza vitanda 50 kwa ajili ya kulaza watoto wanaohitaji matibabu ya moyo.
Waziri Ummy akiwa ndani ya wodi hiyo ya Mwaisela.

“JKCI ni moja wapo ya Taasisi zinazotoa matibabu ya upasuaji hasa ya moyo na ina upungufu wa majengo  hivyo kutokana na uhamishwaji wa wagonjwa jengo la Mwaisela tunawapa nafasi ya kupeleka vitanda 50 kwa ajili ya wagonjwa wao waliofanyiwa upasuaji hususan watoto” aliongeza Waziri ummy.

Pia, alipata muda wa kwenda kumtembelea Mgonjwa alikuwa analalamika kwenye baadhi ya vyombo vya habari ajulikanaye kwa jina la Maria Amrima (17) mkazi wa Masasi Mkoani Lindi kuwa ana uvimbe mkubwa na f kuletwa katika Hospitali ya Taifa yMuhimbili.

“ Niliposikia habari ya Binti huyo kwenye baadhi ya vyombo vya habari niliomba namba za wahusika na kuwaelekeza waende Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hivi sasa anapata matibabu kwenye taasisi ya Mifupa (MOI) na wanaendelea na juhudi za kumtibia ili kumrudsha katika hali yake ya zamani” alisema Waziri Ummy.

Alitoa rai kwa Watanzania kuwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa madaktari bingwa na kuacha imani potofu kwa kwenda kwa waganga wa kishirikina kwa kuamini mgonjwa atakuwa amerogwa ili kuepuka tatizo kuwa kubwa zaidi.


“Kwa mujibu wa madaktari wamesema kuwa Maria alihudhuria hospitali hapo mara mbili na hakurudi tena kama ilitakiwa afanye na badala yake akajikita zaidi kwenye tiba asili mpaka imesababisha tatizo kuwa kubwa zaidi hivyo watanzania tunatakiwa kuwaamini zaidi madaktari na kufuata maelekezo” alisema Waziri Ummy.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement