Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Gloria Leo, akiwaelekeza wananchi waliojitokeza kupata elimu na kufanyiwa uchunguzi, jinsi ya kusafisha eneo la mbele kwa kutumia kifaa maalum.

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

LICHA ya kwamba watu wengi hupiga mswaki hata hivyo imeelezwa hawapigi vizuri inavyotakiwa huku wakidhani kujaza dawa ya kusafisha meno kwenye mswaki ndiyo kusafisha kinywa na meno yao.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo na Daktari Bingwa wa Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gloria Leo wakati alipokuwa akitoa elimu kwa umma kuhusu namna bora ya kusafisha kinywa na meno.
Wananchi wakimsikiliza kwa umakini Dk. Leo (hayupo pichani)

Elimu hiyo imetolewa kwa wananchi waliojitokeza leo hospitalini hapo ambao pia walifanyiwa uchunguzi wa afya ya kinywa na meno bila malipo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno yaliyoanza Machi 13, mwaka ambapo kilele chake ni Machi 20, mwaka huu huko Mkoani Mara.

Dk. Leo amesema dhana hiyo si sahihi na kusisitiza wengi hawajui kusafisha meno na kinywa na hivyo kujikuta wakiishia kuugua magonjwa mbalimbali ya meno hasa kuharibika fizi.

“Kujaza dawa ya kusafisha meno kwenye mswaki hakumaanishi kwamba inasaidia moja kwa moja kusafisha meno yako, kuna jinsi ya kusafisha kinywa na meno kuanzia sehemu ya nje hadi ndani na kukiacha kikiwa kisafi na salama,” amesema Dk. Leo (mwenye MIC pichani).

Amesema katika kliniki yao wanapokea wagonjwa wengi kila wiki ambao wanakabiliwa na magonjwa ya meno na kinywa ambayo wameyapata kutokana na kutojisafisha vema.
Wataalamu wa afya ya kinywa na meno MNH wakimchunguza mwananchi aliyejitokeza kufanyiwa uchunguzi leo.

Amesema jamii inapaswa kubadilika na kujenga utamaduni wa kupima afya ya kinywa na meno mara kwa mara au angalau mara moja kwa mwaka.

“Hiyo itasaidia kama una tatizo linagundulika mapema na unapewa matibabu mapema, usikae nyumbani na tatizo, msitumie dawa ya kusafisha meno mradi mmeona kuwa ni dawa inauzwa, hakikisheni mnanunua dawa ambayo inaonesha ina madini ya floride,” ametoa rai.
Mtaalamu wa afya ya kinywa na meno MNH akimchunguza mwananchi mapema leo.

Picha zote na Veronica Romwald

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement