Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WANAUME wapatao watatu hadi watano kila mwezi katika kliniki ya tiba mazoezi, inayosimamiwa na Mtaalamu wa Tiba ya Mazoezi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk. Frederick Mashili, wakikabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Akizungumza na mtandao huu hivi karibuni, Dk. Mashili alitaja sababu mbalimbali zinazochochea mwanaume kupata tatizo hilo ikiwamo uzito mkubwa.

"Mwanaume anaweza kupata tatizo hilo iwapo ana upungufu wa homoni ya kiume iitwayo testesterone," alisema.

Alisema homoni hiyo wakati mwingine hupungua kutokana na ongezeko la umri au kupungua kwa kiasi na kiwango cha misuli.

"Ikiwa pia kuna upungufu wa damu  inayoingia kwenye mishipa iliyopo kwenye uume, kutokana na kuziba kwa mishipa hiyo mwanaume hujikuta akipata tatizo hili," alisema.

Alisema mishipa hiyo huweza kuziba kutokana na sababu mbalimbali hasa kama kuna kolesto (mafuta) nyingi.

"Sababu nyingine ni matatizo ya kisaikolojia hasa kama ana msongo wa mawazo, Kuna baadhi ya vyakula pia mtu akikosa hasa vile virutubisho muhimu kwa mfano vinavyopatikana kwenye karanga, korosho na vinginevyo huweza kupata tatizo hili.

"Kuongezeka kwa mafuta mwilini huchangia pia tatizo lakini hoja kwamba kujichua husababisha binafsi sikubaliani nayo sana... Kwa sababu naona ni suala la kisaikolojia pia kwamba mtu anapokuwa akitekeleza jambo lile anakuwa ametengeneza taswira ya mtu kichwani mwake, hujiweka kwenye mawazo fulani," alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement