Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image result for born babyNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

Tatizo la jinsia tata liitwalo kitaalamu 'Ambigious Genitalia' huwakabili zaidi wanawake kuliko wanaume, imeelezwa.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zaitun Bokhari alisema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza katika mahojiano maalum na MATUKIO NA MAISHA.

Dk. Bokhari alisema kutokana na wazazi wengi kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo hilo, wamejikuta wakielea watoto wao kama wa kiume kumbe wa kike au kama wa kike kumbe ni wa kiume.

"Kwa mwezi napokea kliniki kati ya watu watano hadi sita wanaokabiliwa na tatizo hili, changamoto ni kwamba hufikishwa wakiwa wamechelewa," alisema.

Alisema ni rahisi kwa mzazi kuweza kubaini iwapo maumbile ya mtoto wake yana kasoro au la!

"Kama mtoto ni wa kike mama akague maumbile yake kwa kuyalinganisha na ya kwake na kama ni wa kiume alinganishe na ya baba yake.

"Yatatofautina kwa ukubwa lakini yatalingana kwa muonekano kama kuna kasoro atagundua tu na iwapo atagundua amuwahishe mtoto wake hospitalini kwa uchunguzi zaidi, vipimo na matibabu," alitoa rai.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement