Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Wauguzi wakiwa katika maandamano ya amani

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

CHAMA cha Wauguzi mkoa wa Dar es Salaam kimeungana na waunguzi wengine duniani kuadhimisha Wiki ya Uuguzi Duniani iliyoanza Mei 6 hadi 12, mwaka huu.

Sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika katika hospitali ya Sinza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Zimepambwa na maandamano ya amani ya wauguzi wa Halmashauri za Manispaa zote tano, yaani Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni na mwenyeji Ubungo.

Wakati wa maadhimisho hayo, wananchi walipata fursa pia ya kupima afya bila malipo ikiwamo upimaji wa Ukimwi, uzito na magonjwa mengine kama vile kisukari.

Wauguzi walipata fursa ya kumueleza mgeni rasmi mafanikio na changamoto wanazokutana nazo kila siku wanapotekeleza majukumu yao.

Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa watumishi katika fani ya uuguzi, kutokupatikana kwa stahiki zao kama posho za masaa ya ziada lakini pia usalama mahali pa kazi na kazalika.

Akizungumza nao, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori aliwapongeza kwa kuwa wanachapa kazi na kwamba serikali ya awamu ya tano inayoongzwa na Dk. John Magufuli inawathamini.

“Na ndio maana tayari imeshatoa kibali cha kuajiri watumishi katika sekta ya afya bila kusahau kwa kadiri uchumi utakavyoimarika ataongeza mishahara minono.
 
“Aidha, amewaagiza wakuu wa wilaya wote na wakurugenzi kuhakikisha wanatatua changamoto zinazowakabili wauguzi,” alisema.

Kwa kuthamini umuhimu wa maisha bora kwa wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makori aliongoza harambee na kufanikisha kukusanya ahadi ya kiasi cha Tsh milioni 4,050,000.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kutunisha mfuko wa Saccos ya Wauguzi huku ofisi yake ya wilaya nayo iki-ahidi kutoa kiasi cha Tsh milioni moja.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo aliahidi kuchangia kiasi cha Tsh milioni moja kutunisha mfuko huo.

Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani kwa Mkoa wa Dar es Salaam yameadhimishwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo katika Hospitali ya Sinza Palestina Jijini Dar es salaam.

Sherehe za maadhimisho hayo huendana na kumbukizi ya Muasisi wa uuguzi Duniani Frorence Nightingale ambaye ndiye kielelezo cha utumishi wa Uuguzi.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement