Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement



Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kifurahia jambo na mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji na kuwekewa mguu wa bandia hospitalini hapo

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameupongeza uongozi na wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT kwa kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Pamoja na hayo amesema bado ipo kazi kubwa kuhakikisha jamii inafikishiwa ujumbe kuhusu tatizo la fistula na athari zake kwa afya ya mama na uchumi kwa ujumla.

Mama Samia amesema hayo leo alipozungumza katika viwanja vya Hospitali ya CCBRT ambako alifanya ziara kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

“Mliponifata kuomba kurekodi ule ujumbe ambao unasambaa mtandaoni kwa njia ya sauti na video hata sikuwa naelewa kwa kina kuhusu tatizo hili, mkanieleza na sikujua kwamba kwa kuzungumza kule kungesaidia kufikisha ujumbe , kumbe imesaidia.

“Lakini bado ujumbe unahitajika kupelekwa kwa jamii siku moja nikiwa kwenye mkutano kule Zanzibar wanawake walinifuata na kunihoji kuhusu tatizo la fistula, nikaanza kuwaeleza, utaona namn ambavyo elimu hii inahitajika zaidi hasa katika ngazi ya chini ya jamii tena ile masikini,” amesema.

Ameongeza “Lazima tuwaelimishe kuhusu umuhimu wa kumuacha mtoto akue ndipo aolewe na kubeba mimba kwani tatizo hili linaepukika ikiwa msichana anaachwa kwanza akue na viungo vyake vikomae tayari kwa kuhimili ile hali ya ujauzito,” amesema.

Awali akizungumza Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans aliiomba serikali kuipunguzia kodi hospitali hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

Akizungumza, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali inakusudia kuirejeshea tena Hospitali ya CCBRT ruzuku kama ilivyokuwa ikipatiwa hapo awali ili kuiwezesha izidi kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na hospitali hiyo katika kuhudumia watanzania na kwamba imekuwa itoa huduma bila kujali faida.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement