Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
NA VERONICA ROMWALD -DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameshangazwa na Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA kwa kitendo cha kusuasua ujenzi wa mabweni katika Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila.

Hayo yamejiri mapema leo wakati makamu huyo wa Rais alipofanya ziara katika hospitali hiyo iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema nyumba hizo zimekusudiwa kujengwa ili kuwawezesha watumishi kukaa karibu na hospitali ili kurahisisha matibabu.

"Lengo la kuharakishwa kwa ujenzi huo kutaiwezesha hospitali hiyo kufanya udahili kwa wanafunzi wengi zaidi na hivyo Serikali itaweza kuzalisha wataalamu.

“Lakini sioni chochote mimi, TBA sijajua nini kinaendelea pale, nikitoka hapa nataka mnipeleke pale nikajue tatizo ni nini na ninawaahidi nitashirikiana na wahusika huku ili nijue suala hili linakwendaje,” amesema Samia.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe, amesema wakati ujenzi huo ukisuasua tayari asilimia 45 ya muda uliotolewa kukamilisha ujenzi huo umepita.

Amesema ujenzi huo unagharimu kiasi cha Sh. bilioni 13.3 na kwamba hadi sasa wameshaipatia TBA kiasi cha Sh. bilioni 3.9 ambazo ni sawa na asilimia 30 ya gharama yote.

Januari 20, mwaka huu, TBA ilipewa kipindi cha wiki moja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ihakikishe inarekebisha mapungufu yaliyopo ili iendelee na ujenzi huo.

Profesa Ndalichako alitoa agizo hilo baada ya kukagua na kushuhudia ujenzi huo ukiwa umesimama huku kukiwa na uchimbaji wa msingi pekee katika majengo manne.

Agosti, mwaka jana TBA ilipatiwa kiasi cha Sh. bilioni 3.9 na Wizara ya Elimu kwa ajili ya ujenzi huo wa majengo saba ambayo yangehusisha mabweni mawili ya wanafunzi, jengo la kufundishia, jengo la maktaba, bwalo la chakula, jengo la maabara, jengo la maabara maalum na jengo la kazi za nje.

Pamoja na hayo, Samia ameahidi kuiongezea fedha za dawa hospitali hiyo Sh. milioni 600 mpaka kufikia Sh. milioni 900 ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa dawa hospitalini hapo.

Ameutaka uongozi kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zitokanazo na dawa ili kuondokana na changamoto hiyo.

Amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kuongeza kiasi cha Sh. milioni 300 ili kuifanya hospitali hiyo iweze kujiendesha na kupunguza changamoto hiyo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement