Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Mwanafunzi bora wa mwaka katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2020, Paul Cosmas Luziga amesema alifunga tatu kavu (bila kula wala kunywa) akiombea mtihani na matokeo yake.

Katika mahojiano maalum na MATUKIO NA MAISHA BLOG, Paul amesema hiyo ni siri ya mafanikio yake na kwamba kila alipoomba Mwenyezi Mungu aliongeza pia juhudi kubwa katika kusoma.

"Nimeokoka Dada, nasali KKKT, huwa naomba mara kwa mara, nafunga na naongeza juhudi kwenye masomo," amesema Paul kwa furaha.

Ameongeza "Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii, ndoto yangu siku moja niwe Injinia (Mhandisi) wa masuala ya mawasiliano.

Matokeo ya kidato cha nne yametangazwa leo, Januari 15, 2021 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde ambapo mwanafunzi huyo ni miongoni mwa wahitimu akitokea Shule ya Sekondari Panda Hill Mkoani Mbeya.

Mama mzazi wa Paul, Lucy Mwogella amesema mtoto wake alikuwa akimtegemea Mungu na familia walikuwa wakimsisitiza kusoma kwa bidii.

Amesema licha ya kuwa na uwezo mdogo kiuchumi, ataendelea kufanya kila awezalo kwa msaada wa Mungu kuhakikisha ndoto za mtoto wake zinatimia.

“Hali yetu ni ya kawaida kwani hatuna wa kumtegemea maana baba yake alifariki tangu mwaka 2018. Kwa sasa Paul anasomeshwa na kaka yake,” amesema Lucy.

Paul amefaulu kwa daraja la kwanza pointi saba huku akiwa na alama “A” katika masomo yote yakiwemo fizikia, kemia, baiolojia na hisabati. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement