Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema - Aliyekuwa Dodoma

Jamii ikiwa na mwamko mkubwa hivi sasa kupambana kupunguza uzito wa mwili ili kuwa na afya njema kwa kutafuta mbinu za kupangilia mlo (diet) na mazoezi kwa afya, Aluta Clinica inakusudia kuweka dawati maalum kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

Hivi karibuni MATUKIO NA MAISHA BLOG ikiwa Jijini Dodoma ilitembelea eneo ambako kutakuwa na kliniki hiyo na kushuhudia maandalizi yakiwa ‘yamepamba moto’ kuelekea ufunguzi wake.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ACS (Afya Courier Services Company), Dk. Wilfred Rutahoile alisema kliniki hiyo ipo eneo la Area C, nyuma / jirani na uwanja wa ndege wa Dodoma.

“Kauli mbiu yetu tunasema ‘ Walk in Care, Your Healthcare Solution’, tunataka mtu aje hapa wakati wowote hakuna ulazima wa kuomba ‘appointment’ ni yeye kuchukua tu hatua zako na kuja kutuona,” alisema.


Dk. Ruta (anayefungua mlango pichani) aliongeza “Aluta Clinica ni sehemu sahihi ya kupata majibu ya afya yako, kutakuwa na elimu ya lishe, jinsi gani ya kupangilia chakula ‘diet’ tunaona watu wanahangaika mno kutafuta elimu huko mitandaoni pamoja na kufanya mazoezi kwa tija ya afya ya mwili.

“Tutatoa elimu, uchunguzi na pale inapohitajika matibabu pia, tunafahamu kwenye jamii wengi huwa tunasherehekea mwaka mpya, lakini hatuna utamaduni wa kuchunguza afya ya mwili, tunataka tuhamasishe jamii, kufanya uchunguzi wa afya mwezi wa kwanza wa mwaka, mwezi wa sita na wa 12.

“Hii itasaidia kuwa na afya njema kwa sababu ikiwa mtu anakabiliwa na magonjwa atagundulika mapema na kupata matibabu mapema, hasa kwa magonjwa yasiyoambukiza, kliniki hii itatoa huduma siku saba kwa wiki kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa mbili usiku,” alibainisha.
 
Aliongeza “Tutakuwa na wataalamu maalum kwa elimu ya mazoezi na kwa upande wa ‘diet’, tunafahamu kuna watu wana shida ya moyo, figo, kisukari wanashindwa kuelewa wale chakula cha namna gani, wasile nini, changamoto ni kwamba kwenye hospitali zetu nyingi hakuna hizo huduma.

“Unakuta tu, kuna kliniki za magonjwa ya moyo, figo, mifupa, wakina mama lakini hakuna kliniki ya lishe, yaani mtu anatoka nyumbani kwake anaenda hospitali kuzungumza na mtaalamu kuhusu lishe tu.

“Tutaruhusu watu waje na familia zao au mpishi wa chakula, tumpe elimu ya lishe au ya kupunguza uzito na madhara yanayotokana na magonjwa mbalimbali yanayohusiana na ulaji, watalipia gharama ya huduma hiyo, tutaweka viwango vya wastani.

“Ni changamoto kubwa ambayo watu wanapambana nayo, mtu anataka kupunguza uzito lakini ale nini, asile nini, mazoezi pia tutakuwa na ‘section’ yake, kwa ajili ya wenye shida za moyo, wenye maumivu ya mgongo, wazee au wasiojiweza,

“Siyo yale ya fiziotherapia bali haya ni yale ambayo tunataka tumuelewehe mtu aweze kuyafanya yeye mwenyewe akiwa nyumbani pale inapotokea anapata maumivu sehemu mbalimbali za mwili.

Aliongeza “Tutatoa pia elimu ya matumizi sahihi ya dawa, watu wanapata changamoto, wengine waandikiwa tu waende kytumia moja mara mbili, ila mfamasia asiwe na muda wa kumuelewesha vizuri.

“Wale wanaopata changamoto hizo kliniki hii itatoa suluhuhiso la matumizi sahihi ya dawa, mtu atakuja na dawa zake hata kama amechukua sehemu nyingine atakuja tutamuelekeza vizuri,

“Dawa inafanya nini maana wapo wengine wamepewa dawa, wanachanganya hawajui za ugonjwa mmoja na mwingine, anapomeza anadhani yote ni ya ugonjwa mmoja lakini kumbe ni magonjwa tofauti tofauti, hakuna kliniki inayosaidia watu kwenye changamoto hii.

“Tunapanga kutoa huduma ya kuhudumia watu ambao wapo nyumbani hawathitaji kuja kliniki, tutatuma watu waende kuwasaidia huko huko waliko, wataonwa na kusaidiwa na ikiwezekana kupelekewa dawa,” alibainisha. 

Alisema wanatarajia kuanza kutoa huduma wakati wowote kuanzia sasa (Januari 2021), ambapo kwa awali itakuwa ya kupilia ‘cash’ na kwamba itapokea bima pale watakapofikia vigezo na kukamilisha mchakato wa kuomba, siku zijazo.
 
“Hivyo, tutaweka gharama ambazo watu wa kawaida wataweza kuzimudu, tunataka tusiwe na mipaka ya wateja ambao tutawapokea, lengo ni kuwasaidia wawe na afya njema,” alisisitiza.
Muonekano kabla ya ukarabati.

Muonekano baada ya ukarabati.

1 Maoni

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement