Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Waziri Gwajima akikagua faili la mgonjwa mmoja aliyelazwa Muhimbili kuona iwapo tayari ameonwa na daktari bingwa kama inavyotakiwa, (mwenye miwani na suti nyeusi pembeni) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru. 

Na Veronica Mrema – Dar es Salaam 

Madaktari Bingwa wenye tabia ya kufika mazingira yao ya kazi, kusaini kitabu cha mahudhurio na kuondoka kusikojulikana bila kuona na kuwahudumia wagonjwa wodini wanavyopaswa, watashughulikiwa kwa mujibu kanuni na taratibu za kimaadili zilizowekwa kisheria.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima ameonesha kukerwa na tabia hiyo akisisitiza kwamba amepokea malalamiko juu ya suala hilo kupitia simu yake ya kiganjani kwa nambari aliyoigawa kwa wananchi.

Mwishoni mwa wiki Dk. Gwajima alitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika moja ya wodi alilazimika kukagua jalada (file) la mgonjwa kuangalia iwapo ameonwa na daktari bingwa au la.

“Nilipokuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya afya tuliwahi kuliona jambo hili, baadhi ya madaktari bingwa walikuwa hawaoni wagonjwa, wakati huo, tuliongea na Prof. Museru (Mkurugenzi Mtendaji wa MNH), alinipa ushirikiano mkubwa.

“Kulikuwa na hiyo tabia, unakuta mabingwa wanasaini, halafu wanapotea kusikojulikana, wagonjwa wanaonwa na madaktari ambao si mabingwa.

“Tukasema haiwezekani lazima tuweke policy (sera) kwamba mgonjwa akishapewa rufaa akaenda hospitali fulani ya kibingwa itamchukua muda gani kuonwa na daktari bingwa,” alisema.

Aliongeza “Ndiyo hospitali hizi zina utaratibu wake kwa sababu zimepewa jukumu la kufundisha, lakini hawa wachache iwe ‘principle’ nchi nzima, kwa sababu nimepata malalamiko baadhi ya wananchi wakinieleza wamekumbana na changamoto hiyo.

“Hapa Muhimbili nimefika, nimefungua mafaili na kuangalia mgonjwa fulani ameonwa lini na bingwa siyo ‘resdent’, nimekuta wapo vizuri.

“Na kwengineko nchini, nimeshawaeleza  wajipange na wameshajipanga, tutaimarisha mfumo kuwe na ‘medical services ‘audit’ kama tunavyo-audit fedha, tuta-audit mifumo yetu mpaka ‘productivity’ (‘uzalishaji’) ya watumishi wetu sekta ya afya na ‘services’ huduma ipoje.

“Kama zinavyotolewa hati safi na chafu kwenye fedha, huku hatutawapeleka hazina bali huko kwenye mabaraza yao ya kitaaluma , wakajadiliwe na kuchukuliwa hatua,” alisisitiza.

Dk. Gwajima aliongeza “Tutaifufua hii mifumo, lengo letu wataalamu wasiogope hizi sheria zao, ni hizo za mabaraza ya kitaaluma tutaziimarisha ili watu waongeze uwajibikaji.

“Siyo jana (juzi), mtaalamu wetu mmoja wa pale wizarani amenitumia taarifa, ameenda mahala fulani naye hajapewa huduma analalamika, tunataka wananchi wote wapate huduma, tunahitaji mabadiliko ya fikra namna ya kufanya mambo,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement