Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Mwandishi Maalum -Dar es Salaam

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imezidi kuchukua hatua na ‘kukunjua makucha’ yake dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, awamu hii inawashikilia watu watatu akiwamo balozi wa nyumba 50, Mtaa wa Juwaje, Kunduchi Pwani, Kulwa Shamas (49).

Shamas anashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo, watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa ni Adadhati Mchongeza(20) na Emmanuel Msakuzi (23).

Mchongeza na Msakuzi walikamatwa kwa pamoja na maafisa wa DCEA wakiwa wameifadhi dawa aina ya heroin zenye ujazo wa gramu 400 pamoja na majani ya bangi puli moja katika  mfuko wa nailoni.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, James Kaji amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipozungumza katika mkutano na waandishi wa habari.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa Januari 22 mwaka huu katika eneo la kunduchi Pwani, Kauzeni Jijini humo wakiwa na unga unaodhaniwa kuwa dawa za kulevya aina ya heroin sambamba na majani makavu ya bangi puli moja sawa na kete 30 za bangi.

Amesema maafisa wa DCEA walifanikiwa kufanya upekuzi hatimaye kukamata dawa za kiasi cha dawa hizo zikiwa zimeifadhiwa ndani ya mfuko wa nailoni.

Kamshina Jenerali Kaji amesema Mamlaka hiyo inaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao na kwamba watafikishwa  mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka hiyo ili DCEA iendelee kufanya kazi ya kukomesha vitendo hivyo.

Pamoja na hilo, Kamshina Jenerali Kaji amesema katika kipindi cha  mwezi Novemba mpaka Disemba mwaka jana DCEA imefanikiwa kushinda kesi  tatu mahakamani zinazohusisha mapapa wa dawa za kulevya nchini ambao wamefungwa jela kwa miaka tofauti tofauti.

Ametaja majina ya mapapa hao ni pamoja na mfanyabiashara maarufu Jijini Tanga Yanga Omary Yanga maarufu Rais wa Tanga na kuhukumiwa miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin uzito wa gramu 1052.63

“Mwingine ni Ayubu Mfaume maarufu kiboko ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kusafirisha heroin zenye  uzito wa gramu  251.25,” amebainisha.

Ameogeza “Watuhumiwa wengine ni Raia wa Iran ambao walitiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye ujazo wa gramu 111.02 katika bandari ya Hindi ambapo mpaka sasa wanatumikia kifungo cha miaka 30.

Vilevile amesema DCEA imefanikiwa kufungua vituo vitatu vya kutolea tiba ya methadone katika mkoa wa Tanga , Bagamoyo, pamoja na hospital ya Tumbi Pwani.

"Mamlaka imeogeza wigo wa upatikanaji wa tiba ya uraibu wa dawa za kulevya kwa kuongeza vituo vingine vitatu vya kutolea tiba ya methadone"amesema Kamshina Jenerali Kaji.

Ameongeza “Vituo hivyo vipo katika maeneo ya Segerea, Mbagala Rangi Tatu na Tegeta vinatarajiwa kuanza kutoa huduma Februari mwaka huu .

Amesema mpaka sasa DCEA inaendelea Kudhibiti vitendo vinavyojiusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kiasi kikubwa.

"Sisi hatuna mchezo katika suala la kukamata watu wanaojiusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya tukikumata unakwenda jela,"amesisisitiza Kamshina Jenerali Kaji.

Amesema vile vile DCEA inaendelea kutoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya kwa njia mbalimbali ikiwemo matukio makubwa ya kitaifa pamoja na vyombo vya habari.

"Mamlaka imeandaa mwongozo wa uelimishaji kwa wadau wanaofanya uelimishaji kwa makundi mbalimbali ya kijamii unaotarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa fedha," amebainisha.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement