Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dk. Moshiro akitoa maelezo kwa Waziri Gwajima jinsi wanavyowahudumia watoto waliozaliwa kabla ya kutimiza muda wa kuzaliwa, ambapo pia alitembelea wodini walikolazwa pacha hao.

Na Veronica Mrema – Dar es Salaam

Pacha wengine waliozaliwa wakiwa wameungana huko Mkoani Iringa na wengine kutoka Shinyanga wamepokewa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hivi karibuni.

Mwishoni mwa wiki, wakati wa ziara yake hospitalini hapo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima aliwatembelea pacha hao wodini walimolazwa.

Akizungumza Daktari Bingwa wa Watoto wa Muhimbili, Robert Moshiro, alimueleza Dk. Gwajima kwamba miongoni mwa pacha hao wapo ambao wanahitaji huduma ya ubingwa wa juu ya upasuaji kuwatenganisha.

“Tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Saudi Arabia ambao wameonesha nia ya kuwafanyia upasuaji pacha hao, ni ‘complex issue’ hawa wa Iringa, wa Shinyanga inabidi tuendelee kuwakuza kwanza ili kuweza kuangalia uwezekano iwapo nao watatenganishwa kwa upasuaji au la, hawa bado ni wadogo,” alisema.

Dk. Gwajima aliwapongeza Muhimbili kwa hatua hiyo ya kuwasiliana na wenzao wa Saudi Arabia ili washirikiane juu ya pacha hao.

Alisisitiza anafahamu idara hiyo inajitahidi kupambana kwa kila namna kuhakikisha watoto wachanga wapata huduma bora ikiwamo pia wale waliozaliwa kabla ya kufikisha umri wa miezi tisa (njiti).

Waziri huyo aliwapongeza Muhimbili hususan kitengo hicho kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya usiku na mchana kuhakikisha wanaokoa uhai wa watoto wachanga wanaofikishwa kwao.

“Nafahamu kazi nzuri mnayofanya, hongereni mno, nilishawahi kuja hapa usiku, kama vile niliwavamia enzi hizo, niliona jinsi mnavyofanya kazi kubwa na ngumu, nitatenga siku maalum nije kwa ajili ya kuzungumza nanyi kwa kirefu,” alisema.


Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement