Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Wetu - Tanga

Wataalamu mabingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), wameendesha mafunzo maalum ya uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwa watoa huduma za afya kutoka wilaya zote za Mkoa wa Tanga.      

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa ORCI, Dk. Crispin Kahesa amsema mafunzo hayo ni ya siku sita na kwamba yamefunguliwa rasmi leo Januari 25 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Jonathan Denemu.

Dk. Kahesa amesema jumla ya watoa huduma 25 kutoka katika vituo vya afya na hospitali 20 mkoani humo, wameshiriki mafunzo hayo. 

"Mafunzo haya yatawapa uwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kutumia Tiba Baridi (Cryotherapy)," amebainisha.

Amesema mafunzo hayo yanaenda sambamba na Kampeni ya Uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi itakayofanyika mkoani hapa kuanzia Januari 28 hadi 30, 2021, Hospitali Rufaa ya Mkoa Tanga - Bombo.

Dk. Kahesa amebainisha kwamba mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais. Samia Hassan Suluhu wakati wa mbio za hisani za NBC Marathon zilizofanyika Dodoma, Novemba 22, 2020.

Amesema kutokana na mbio hizo Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ilipokea ufadhili wa NBC wenye lengo la kufundisha watoa huduma 100 nchini Tanzania.

"Natoa rai kwa wakazi wa Tanga, wanawake wafike kwenye kambi hii ya uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya kizazi ili tuweze kuwahudumia, saratani ikigundulika katika hatua za awali ni rahisi kutibika na kupona kuliko mtu anapochelewa," ametoa rai.

Mafunzo yakiendelea mapema hii leo.
Mafunzo yakiendelea mapema hii leo.

Mafunzo yakiendelea mapema hii leo.





Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement