Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema – Mwanza
 

Si aina zote za dawa mgonjwa anapomeza huzuiwa kutumia (kunywa) maziwa, baadhi ya dawa inashauriwa wazi wazi kutumia maziwa kwani husaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wake kwa mfano dawa mseto ya malaria (ALU).

Yalibainishwa hayo hivi karibuni na Mchunguzi wa Dawa wa Maabara ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) – Kanda ya Ziwa, Lameck Kapilya (pichani) alipokuwa akifafanua jinsi wanavyochunguza myeyuko wa viambata hai vilivyomo ndani ya dawa ili kufanikisha tiba, kwa kutumia mashine maalum iitwayo Dissolution Machine (inayoonekana pichani).

“Ikitokea mgonjwa amemeza dawa na kutapika pale pale, inabidi ameze dawa nyingine, hapo inakuwa haijafika popote, baadhi ya dawa tunashauri zitumike sambamba na maziwa kwa sababu husaidia ule utendaji kazi wake,” alisema.

Alifafanua “Kwa mfano dawa mseto ya malaria (ALU) mgonjwa anashauriwa kunywa maziwa kwa sababu zenyewe zinahitaji 'fat' kuimarisha utendaji kazi wake.

“Lakini zipo baadhi ya dawa ambazo mtu anapozitumia hapaswi kunywa maziwa kwa sababu husababisha utendaji kazi wake usiwe mzuri, hivyo lazima ushauriwe na daktari,” alisema.

Mchunguzi huyo alisema vile vile hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba unywaji wa soda sambamba na dawa huweza kusababisha kifo kwa mtumiaji husika.

“Kile ni chakula hakuna ‘effect’ yoyote inawezekana mtu alikuwa na tatizo jingine, kwa mfano anaweza kumeza dawa akazidisha au ikaenda kukutana na tatizo jingine ikamletea shida, mule ndani kuna ‘Carbonate’ ambayo hutibua ‘asidi’ mule ndani ndiyo maana mtu mwingine anaweza kujihisi vibaya, lakini si kusababisha kifo,” alibainisha.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement