Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum - Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, ameshangazwa kusikia wagonjwa hawapewi Paracetamol lakini alivyotembelea stoo akakuta dawa hizo zipo. 

Dk. Gwajima amekutana na hayo huko katika Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Mkoani Mwanza akiwa ziarani.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Afya ameshangazwa pia namna mnyonyoro wa dawa unavyoendeshwa hospitalini hapo.

"Inaonekana kuna uzembe na ubadhirifu mkubwa wa dawa na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali," amesema.

Dk. Gwajima amekemea vikali tabia ya watumishi wa sekta ya Afya kudanganya na badala yake  amewataka kuwa weledi katika utumishi wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akiwa ziarani, ameweka wazi kwamba amebaini kuwepo malalamiko ya uhaba wa dawa kutoka wananchi yaliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Cornel Magembe.

"Nimekaa hapa dakika tano tu, mmenidanganya mpaka kule kwenye damu," amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement