Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Wasichana hao wakiwa katika picha ya pamoja na baba wa Valentina, Rwegasira, hivi karibuni.

Na Veronica Mrema 

Wasichana watatu Valentina Rwegasira (18)  Zainabu Kambona (19) na Zuwena Peter (18) wamepata alama za daraja la kwanza katika matokeo yao ya kidato cha nne, yaliyotangazwa hivi karibuni na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Charles Msonde.

Wasichana hao waliomaliza masomo yao ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Zanaki siku kadhaa zilizopita katika mahojiano maalum na MATUKIO NA MAISHA BLOG walieleza kwamba wana ndoto ya kuwa madaktari bingwa wa magonjwa ya damu kwa upande wa siko seli.

Matokeo yao ambayo MATUKIO NA MAISHA BLOG imeyaona Valentina Rwegasira amepata I:8  Zainabu Kambona I:10 na Zuwena Peter  amepata I:13.

Wasichana hao katika mahojiano na mtandao huu walisisitiza kwamba wataendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na wao watazidisha juhudi katika kujifunza wafikie ndoto yao hiyo.

Katika matokeo ya kidato cha pili,  Valentina alisema aliipata I:7 na matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mock alipata I: 9.

Zuwena alisema kidato cha pili alipata 1:10 na kidato cha nne katika mtihani wa 'mock' alipata 1:13.

Zainab naye alibainisha kidato cha pili alipata I:9 na katika ‘Mock’ kidato cha nne alipata I:13.

Mtafiti Bingwa wa Magonjwa ya Damu na mbobezi kwa zaidi ya miaka 20 katika ugonjwa wa siko seli, Prof. Julie Makani amewapongeza wasichana hao.

Kwa undani zaidi tafadhali tembelea link... https://matukionamaisha.blogspot.com/2021/01/simulizi-ya-wasichana-watatu-vipanga-wa.html

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement