Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Wananchi wakikipiga picha ya kumbukumbu na samaki huyo.

Na Veronica Mrema

Samaki wa baharini anayetajwa kuwa na ‘utajiri mkubwa’ katika kusaidia kuongeza nguvu za kiume, amenogesha banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, maonesho ya 46 ya biashara ya Kimataifa {sabasaba}.

MATUKIO NA MAISHA BLOG imeshuhudia wananchi wakimshangaa samaki huyo huku wengi wakiomba kumshika ili kupiga naye picha za ukumbusho.

Akizungumza, Ally Makame ambaye ni miongoni mwa Maafisa wa Abajuko Enterprises ambao ndiyo waliokuwa wamepewa dhamana ya kuonesha samaki huyo na baadhi ya samaki wengine kwenye maonesho hayo, amesema wananchi wengi wamevutiwa naye.

“Tumeonesha samaki ‘live’ {yaani wakiwa hai kabisa}, kuna mkunga, kamba kochi, kaa na hawa wanaoweza kuongeza nguvu za kiume, huyu bei yake kwa sasa inaanzia 150,000 na wanauzwa kwa kilo na hawa kaa wao bei yao ni 15,000.

“Soko lake mara nyingi ni nje ya nchi, tunawachakata kiwandani, tunapeleka nje kwa sababu soko la ndani bado mwamko ni mdogo, mtu ukimuambia anauzwa 150,000 na wengi vipato vyetu ni vya hali ya chini, hawanunui.

Ameongeza “…, wanauliza nyama yake ipoje {kwa sababu si kipande kikubwa mno}, hivyo ukimuonesha anasema kinyama hicho tu ndiyo bei hiyo, hawanunui.

“Samaki huyu ana uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kwa sababu ana madini mengi ya zinki, hata wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu huwa wanashauriwa angalau kwa siku wale kipande kimoja,” amedai.

Ameongeza “Samaki huyu kwenye hoteli kubwa kubwa huko kipande kidogo unaweza kukuta kinauzwa hata 170,000 na kuendelea, menu yake ni ghali.

Afisa huyo akionesha aina nyingine ya samaki aitwaye Mkunga ama nyoka wa baharini, analiwa lakini ana uwezo wa kung'ata kama nyoka wa kawaida.

Picha zote na Veronica Mrema

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement