Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Watu 296 duniani waligundulika wanaishi na Homa sugu ya Ini kirusi aina B mwaka 2019 ambapo zaidi ya nusu {66%} ya maambukizi hayo yalitoka Bara la Afrika, limeripoti Shirika la Afya Duniani {WHO} ripoti ya Homa ya Ini ya mwaka 2021.

WHO limeeleza, kipindi hicho watu wapatao milioni 58 walikuwa wanaishi na maambukizi ya Homa ya Ini kisuri aina C na wakati huo huo kulikuwa na vifo 820,000 duniani ambavyo vilisababishwa na Homa ya Ini kirusi aina B.

Yameelezwa hayo kupitia tamko la Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa Umma kuhusu Siku ya Homa ya Ini duniani inayoadhimishwa ifikapo Julai 28, kila mwaka {leo}, lengo kuelimisha  na kuikumbusha jamii kutambua athari za ugonjwa huo, unavyoambukizwa na jinsi ya kujikinga.

“Kwa Tanzania, takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) zinaonesha kuwa maambukizi ya Homa ya Ini aina ya B miongoni mwa wachangiaji damu kwa miaka mitatu ni kama ifuatavyo mwaka 2018 (4.4%), mwaka 2019 (5.9), mwaka 2020 (6.1%) na mwaka 2021 (5.3%).

“Aidha, kwa kipindi hicho maambukizi ya Homa ya Ini aina C yameendelea kuwa ni ya 2.3%,” amebainisha.

Amesema Ugonjwa wa Ini aina ya A na E unaweza kuzuilika kwa kuboresha usafi wa mazingira, utayarishaji wa vyakula katika hali ya usafi na matumizi ya maji safi na salama.

Amesema Ugonjwa wa Homa ya Ini aina ya B, C na D inazuilika kwa kutekeleza afua zote za kuzuia virus vya VVU/UKIMWI.

“Kwa virusi aina ya B ipo chanjo ambayo hutolewa kwa utaratibu wa kawaida wa utoaji wa chanjo kwa watoto wachanga. Chanjo hii ilianza kutolewa kwa watoto nchini waliozaliwa kuanzia mwaka 2002 (Pentavalent).

“Kwa kipindi cha mwaka 2021 utoaji wa chanjo ulifikia kiwango cha asilimia 98 ya watoto wote chini ya miaka mitano walipata chanjo ya Pentavalent. Hakuna chanjo dhidi ya Homa ya Ini C, D na E.

“Chanjo ya watu wazima hutolewa kwa watu walio kwenye makundi hatarishi. Makundi hatarishi kwenye maambukizi ya Homa ya Ini aina B na C ni Watumishi wa afya.

“Wanaume wanaofanya ngono na Wanaume wenzao, Watu wanaojidunga madawa ya kulevya, Watu wenye wapenzi wengi, watu wenye magonjwa sugu ya Ini, figo, kisukari na wenye upungufu wa kinga mwilini,” amesema.

Amesema matibabu ya Homa ya Ini hufanyika kulingana na aina ya maambukizi.

“Kwa wagonjwa waliopata virusi aina ya A na E, tiba yake mara nyingi hutolewa kutokana na dalili zinazoambatana na ugonjwa huu,” amesema.

Ameongeza “Kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na Homa ya Ini B matibabu hutegemea hatua ugonjwa aliyofikia, na wakati mwingine mgonjwa hulazimika kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa huo kwa kipindi chote cha uhai wake.

“Kwa upande wa Homa ya Ini aina ya C tiba ipo na inachukua muda wa miezi mitatu hadi sita kukamilisha matibabu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement