Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema - Dar es Salaam

Homa ya mgunda si tishio tena la ki-afya kwani wataalamu na wanajamii Kusini mwa Tanzania wameweza kuidhibiti ipasavyo, hakuna kisa chochote kipya  kilichoripotiwa.

Yameelezwa hayo leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mbele ya Waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo ndani ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu {NIMR}.

Waziri Ummy amesema tangu Julai 18, 2022 Wizara hiyo ilipotoa taarifa hadi kufikia sasa idadi ya waliougua imesalia watu 20 na vifo ni vile vile vitatu vilivyotokea awali.

"Habari njema ni kwamba, timu yetu ya ufuatiliaji imebaini hata watu ambao walitengamana {walikaa karibu zaidi na wagonjwa hao} wote hawana ugonjwa," amesema.

Ameongeza "Hawana dalili wala maambukizi ya ugonjwa huu, hadi sasa... Hii inadhihirisha kwamba ni mara chache mno hutokea ugonjwa huu kuambukiza kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwengine.

"Watu 15 wenye umri kati ya miaka 11 hadi 70 waliotengamana na wagonjwa hao ndiyo ambao walifuatiliwa kwa ukaribu," amebainisha.

Waziri Ummy amesisitiza "Wataalamu wetu wanaendelea na utafiti wa kina kwa binadamu na wanyama na mazingira yanayowazunguka ili kuweka mikakati zaidi ya udhibiti.

"... na juzi Waziri Mkuu {Kassim Majaliwa} alituagiza kwamba ipo haja kuimarisha dawati moja la afya humo zipo sekta ya afya, mazingira, mifugo, wanyama, kilimo na maji. 

Amehimiza jamii kuendelea kuimarisha usafi mazingira ikiwa ni pamoja na kunywa maji safi na salama.

"Licha ya kwamba mara chache huambukizwa kutoka kwa binadamu mmoja na mwingine ni muhimu kuchukua hatua kuepuka maji au vitu vilivyochaguliwa na wanyama kunywa.

"Kunywa maji yaliyochemshwa na wenye dalili za homa kuvuja damu kichwa kuuma na mwili kuchoka wafike vituo vya afya mapema ili wapate tiba stahiki.

Ameongeza " Maana wale wawili wa mwanzo walichelewa tukashindwa kuokoa maisha yao waliofika mapema walitibiwa na kurudi nyumbani mapema.

"Wizara inawaomba wananchi watoe taarifa za wagonjwa wenye dalili hizo ... Na timu za ufuatiliaji wa magonjwa watoe taarifa kwa wakati.

Amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya waimarishe na kufufua timu hizo za ufuatiliaji wa magonjwa na wafuatilie tetesi yoyote ya ugonjwa unaodaiwa kuzuka nchini.

"Kwenye afya ya jamii ... ukisikia pale mtoto ametoka mapele kama homa ya nyani ni wajibu wetu kufuatilia, awahi kituo cha afya tuchukue sampuli na kujua ni ugonjwa gani. Tutaiweka nchi na dunia salama.

Ameongeza "Lakini kwa sasa wananchi wasiwe na hofu, hatutatoa taarifa kwa umma kuhusu ugonjwa huu {Homa ya Mgunda} kwa sasa labda pale itakapojitokeza.

"Tutaendelea kutoa taarifa za magonjwa mengine kama kawaida kupitia mifumo yetu kama vile UVIKO - 19, kipindipindu na mengineyo kwa ngazi ya Kimataifa kwenye Shirika la Afya Duniani {WHO}.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement