Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

 Montreal , Canada

Tanzania kupitia Wizara ya Afya itaendeleza kuimarisha ushirikiano wake na mahusiano mema na Global Fund ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa makini miradi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amemuhakikisha hayo Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund Bw. Peter mapema hii leo walipokutana na kufanya mazungumzo hapa Montreal nchini Canada ambako unaofanyika Mkutano wa Kimataifa wa UKIMWI.

Katika mazungumzo hayo Prof. Makubi amemuhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Wizara ya Afya  itaendelea kuboresha zaidi huduma za afya kwa wananchi.

Katika Mkutano huo Tanzania imewasilisha 360 video ya mafanikio ya mfuko wa  Serikali na Global Fund katika kudhibiti magonjwa ikiwemo UKIMWI, Malaria, TB na kuimarisha mifumo ya Afya. 

Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund ameahidi  kutembelea Tanzania mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement