Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema – Kilimanjaro

Vyombo vya habari vitakavyozingatia usawa wa kijinsia pamoja na kushajihisha masuala ya kijinsia vina nafasi kubwa ya kudumu kwenye sekta ya habari kuliko vile visivyozingatia.

Yameelezwa hayo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania{MCT}Kajubi Mukajanga, alipozungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tatu ya masuala ya wanawake na uongozi yanayofanyika Mkoani hapa.

“Mafunzo haya ni ya awamu ya tano katika mtiririko wa mafunzo ya aina hii tangu mwaka 2019 kwa mara ya kwanza tulifanya Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar na sasa Kilimanjaro,” amebainisha.

Amesema MCT inafanya mafunzo hayo kwa sababu imani yake ni katika ussawa wa kijinsia.

“MCT inaamini vyombo vya habari vitakavyodumu ni ambavyo vitazingatia jinsia na kushajihisisha jinsia katika maudhui yake itakayoandika na kurusha,” amesisitiza.

Mukajanga ameongeza “Imani yetu ni kwamba huwezi kuacha nusu au zaidi ya nusu ya wateja wako nyuma na ukawa na maendeleo.

“Kwa hiyo MCT ilipitisha hii program ya jinsia miaka mitatu iliyopita na tumeweza kuipa kipaumbele kama sehemu muhimu na mahususi ya vyombo vyetu.

Amesema mkakati huo ulioanza 2019 utakaohitimika 2025 umelenga angalau kila mwaka kufikia wanahabari wanawake 24 kwa mafunzo hayo.

“Lakini kitu muhimu ni kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake {baada ya mafunzo haya} akahakikishe anatimiza wajibu wake, ukishikwa shikama,” amewaeleza washiriki wa mafunzo hayo.

Ameongeza “Tutahitaji mrejesho, je umesaidikaje na umesaidiaje wenzako, umepata ‘promotion’ kwa hiyo msikilize mawasiliano vizuri.

Amesema MCT inatoa mafunzo hayo kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Vyombo vya Habari la nchini Finland akisisitiza lengo mahususi ni kujenga uwezo wa kuwapo usawa wa kijinsia katika vyombo vya habari nchini.

Awali, washiriki 24 wa mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam, Tabora, Iringa, Manyara, Zanzibar na mengineyo, walikaribishwa na mwenyeji wao, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro, Bahati Nyakiraria.

Akizungumza, amesema wanahabari wanawake wakijiamini wana uwezo wa kufanya mambo makubwa yatakayoleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali.

“Mjenge kujiamini mtafanya makubwa, kuweni imara na wenye uthubutu, mjiamini mtatenda makubwa na mtaleta mabadiliko,” amesisitiza.

Ameweka wazi kwamba hivi karibuni ataanzisha kituo cha redio na kundi la wanawake atalipa nafasi kwani anaamini wana uwezo pia katika utendaji kazi huku akiwasisitiza washiriki hao kuzingatia vema mafunzo hayo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement