Moyo nimeufungua, Tayari kuwaandikia.
Karibuni mjongee, Wake na waume pia,
Wasichana na Vijana, My wenu nawaeleza.
Ugonjwa Siko Seli, Bado wengi hamjui,
Si laana ya vizazi, Wala ndumba za wachawi.
Ni ugonjwa wa kurithi, Kwa vinasaba vya wazazi,
Wote baba na mama, Mtoto wanapomtengeneza.
Mimba inapoingia, baba na mama humpa,
Kinasaba cha ugonjwa, Kiumbe tarajiwa.
Si ugonjwa wa kuambukiza, Daima hili kumbuka,
Usimtenge mgonjwa, Usimfanyie unyanyapaa.
11,000 kila mwaka, Huzaliwa na ugonjwa.
Ni kati ya mataifa, yenye wengi wagonjwa,
Barani Afrika, Dunia nayo inajua.
Siko Seli huchangia, Vifo vingi vya watoto,
Chini ya 5 miaka, Kila mwaka Tanzania.
Uhai wakijaliwa, Maumivu ni makali,
Huyaishi daima, Kila siku ya maisha.
Damu kwisha mwilini, Na mateso mengi pia,
Hupitia kila mara, Kuugua na kulazwa.
Kuuvunja mduara, Vijana tuna dhamana,
Kabla ya kuanza ndoa, Watoto kuwaleta.
Muhimu chunguza afya, Hali yako ya kinasaba,
Umerithi ama la, Amua kwa busara.
Ikiwa una kinasaba, Chagua asiye nacho,
Hii ndiyo njia bora, Kuuvunja mduara.
Hapa natamatika, Ujumbe nimeufikisha,
Sina shaka umeelewa, Hatua chukua sasa.
Veronica Mrema
M24 TANZANIA MEDIA
VRM19062024
Chapisha Maoni