Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


IsdoryMwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Luis, James

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

SHULE ya Msingi Mbezi Luis imepatiwa Sh milioni 63 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa inayokabili shule hiyo.

Akizungumza juzi na wazazi kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya shule hiyo,  Mwenyekiti wa Kamati ya shule,  Willium Musiba alisema fedha hizo zilitolewa na Rais John Magufuli.

"Kama mnakumbuka Rais Magufuli alipunguza mshahara wake na mawaziri wake na akazipeleka moja kwa moja ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  tunashukuru Luis tumepata mgawo huo kwa ajili ya madarasa matatu, " alisema.
 

Alisema kujengwa kwa madarasa hayo kutafanya jumla ya madarasa sita yatakayotumika kwa wanafunzi zaidi ya 800.

"Pamoja na hayo tulipata pia Sh milioni 7.8 ambazo zimetolewa kukarabati madarasa ya manne na moja linalotumika kama ofisi ya walimu.  Na bado katika mwaka huu wa fedha tunatarajia kupata fedha nyingine kwa ajili ya kujenga madarasa mengine matatu na ofisi ya Mwalimu Mkuu "alisema.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mbezi Luis,  James Isdory alisema amepanga mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha wananchi kuchangia Sh 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa la awali.

" Tumepata fedha hizo za madarasa matatu lakini lazima tuwe na darasa la awali ni vyema nasi tuchangie maendeleo haya ikizingatiwa kwamba tayari benki ya NMB imeahidi kutupa Sh milioni 5 ya vifaa vya darasa hilo, " alisema.
 




Diwani wa Kata ya Mbezi Luis, Humfrey Sambo akizungumza na wananchi katika moja ya mikutano yake

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Agrey Mwakisole alisema ina jumla ya wanafunzi 890 huku changamoto nyingine ikiwa ni maji safi ya kutumia.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement