Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
http://www.docsciences.fr/IMG/jpg/pacemaker2.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
 
TEKNOLOJIA inazidi kukua kadri miaka inavyosonga mbele. Wataalamu wa sayansi nao wanazidi kubuni vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kurahisisha maisha. 

Kila siku vitu vipya vimezidi kuvumbuliwa katika ulimwengu huu, katika sekta tofauti tofauti ikiwamo sekta ya afya. 

Pacemaker au maarufu nchini kama betri ya moyo ni miongoni mwa vifaa ambavyo vimebuniwa katika ulimwengu huu. 

Kwa mujibu wa wataalamu, Kifaa hiki ni maalumu na kwamba huwekewa mtu
ambaye moyo wake unashindwa kuzalisha umeme wa kusukuma damu kwenda
kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgj9qLKpDN3xWkVKZz8ZTvbJ-9hBlNu3PEwKsooQKR5MV2C_4dqpyrYlDcruJEi7ca59bQwVCpeqsFw6MLSy3EynT8M3OwR0ioa6jSl4gHZgkvE5p0Xy4aQ6wZ7zwBaXS3W6ZQQ5X-QS_T7/s1600/61.jpg 

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi.

Inaelezwa kwamba kwa mara ya kwanza kilianza kuwekwa katika mwili wa binadamu mnamo mwaka 1960. 

Lengo la kuwekwa kwa kifaa hicho katika moyo wa binadamu ni kuwezesha kuzalishwa kwa umeme ili kusaidia kusukuma damu katika moyo unaoshindwa kusukuma kwa kutumia umeme wa asili. 

Julai 15, mwaka huu Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ilifanikisha kufanya upasuaji wa kupandikiza kifaa hicho katika moyo wa mtoto Happiness Josephat (6). 

Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa katika Taasisi hiyo,  Happiness alizaliwa na tatizo linalojulikana kwa kitaalamu 'heart brock'.
https://aos.iacpublishinglabs.com/question/aq/700px-394px/functions-pacemaker_ba433f11e5804ef4.jpg?domain=cx.aos.ask.com Kwamba moyo wake ulikuwa hauzalishi umeme wa asili kuwezesha misuli yake kusukuma damu kwenda kwenye sehemu nyingine za mwili wake.
 
Happiness alizaliwa Desemba 16, mwaka 2010 huko wilayani Mbulu mkoani Manyara. Alikuwa akipoteza fahamu kila siku mara nne hadi sita. 

Upasuaji wake ulifanyika kwa mafanikio ambapo Agosti mosi, mwaka huu
aliruhusiwa kurejea nyumbani, hata hivyo hali yake ilibadilika ghafla siku kadhaa kabla ya kurudi kliniki kwa uchunguzi zaidi katika Taasisi hiyo.

http://www.richardmwambe.com/wp-content/uploads/2016/03/images-ds.jpg 

 Kwanini watoto huzaliwa na tatizo hilo.
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto, Godwin Sharau anasema watoto 20000 huzaliwa na tatizo kama lile la marehemu Happiness kila mwaka. 

Anasema watoto wengi hupata ugonjwa huu hutokana na ile nguvu ya kupiga maradhi ya mama ‘auto immune’ pale inapovuka katika kondo la mtoto wakati akiwa tumboni. 

"Mtoto anakuwa ametungwa na moyo mzuri lakini zile nguvu za mama (antibody) zinavuka na kuingia kwenye damu ya mtoto na kusababisha huaribifu ‘heart brock’, " anasema. 

Anasema iwapo itatokea hali hiyo ya antibodies kuvuka katika kondo la uzazi na kumfikia mtoto husababisha karibu asilimia 70 ya watoto hawa kufia tumboni.
 
"Asilimia 25 pekee ndiyo hubahatika kuzaliwa hata hivyo kati ya hao asilimia 85 katika mwezi wa kwanza hufa.
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3187578/highRes/1319129/-/maxw/600/-/yjll5w/-/uPASUAJI.jpg Madaktari wakifanya upasuaji

"Hii ni kwa sababu ule uwezo wa moyo kusukuma damu mbele si mzuri, wanaopona ndiyo huwa kama marehemu Happiness kwetu JKCI ilikuwa jambo la ajabu kumpata mtoto yule.
 
"Watoto wengi hupoteza maisha kabla ya kufika hospitalini , kwa watu wazima inatokea sana na wengi huwekewa vifaa hivi, " anasema.
 
Anasema katika taasisi hiyo tayari wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa
kupandikiza betri wagonjwa 31.
 
Historia ya kifaa hicho
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQGDG1yxamG3PIX8pdEZRAiAVlOx5J9lzpr3NcKma0T-MYfCuPPjWlzjovFOmrQI0OO7oWVv1JceW8IkINTmw58dyb1gSzqUl569K37f9BwnUmVU3ik-3E2or4GR14VVynbCeBSDM04RVj/s1600/2.JPG Daktari huyo (katikati juu) anasema Pacemaker, ni kifaa maalumu ambacho huwekewa mtu ambaye moyo wake unashindwa kuzalisha umeme wa kusukuma damu kwenda kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
 
Anasema ni vifaa vinavyowekwa mwili tangu 1960 kwenye mwili wa binadamu, watu wasiopungua milioni 3, kila mwaka watu wapatao 600,000 huwekewa kifaa hicho.
 
Anasema hadi sasa watu wapatao milioni tatu tayari wamekwisha wekewa kifaa hicho duniani.
 
“Miongoni mwa watu mashuhuri waliowekewa kifaa hicho ni Sir Alex furgerson, ameishi nayo kwa miaka 10 sasa, mwigine ni Elton John ambaye aliwekewa tangu mwaka 1999, huyu alikuwa kwenye safari ya kwenda kwenye sherehe ya David Beckam.
https://1.bp.blogspot.com/-0mQAdbXtI3Q/V0YU-xF5awI/AAAAAAAIqJU/0YPefjn7tKA20-amMq1Th09trIGdsdzXACLcB/s640/160525142810_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_640x360_bbc.jpg “Alipofika uwanja wa ndege alijisikia vibaya walipompima iligundulika kuwa mapigo yake hayafanyi kazi vizuri hivyo alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa hicho,” anasema.
 
Anasema wagunduzi wa kifaa hicho wanaendelea kukiboresha kila wakati.
 
"Miongoni mwa vitu vinavyoboreshwa ni ule uwezo wa nguvu inayowekewa ndani ili iweze kudumu muda mrefu na bado wanaendelea kuboresha.
 
Ushuhuda wa mgonjwa
 
Profesa Gerard Msananga wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kitengo cha Afya ya Jamii ni miongoni mwa watu waliowekewa kifaa hicho katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI).

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggvqUBZjR1W-deX8P0R-owsmqyJJ2sFtQJWgdNQ-d305TnMMRUvobx2zjaq_Qrph9r9sywwMoDPz8a07BoaAGjpQ8YhOQ3Jg4G9naNHtqP4INqwOMyLyVIJ_3wsypv845erEIPsdTga-rP/s2560/%25255BUNSET%25255D.jpg Anasema aligundulika kuwa na tatizo la moyo mnamo mwaka 2010 naada ya kufanyiwa vipimo hapa nchini.
 
“Nilipogundulika kuwa na tatizo hilo, nilikwenda nchini India kwa matibabu zaidim, kule nilifikia katika Hospitali ya St Jude, ambapo nililazwa kwa matibabu,” anasema.
 
Profesa Msananga anasema Februari 2011, aliambiwa kwamba alihitajika kuwekewa kifaa hicho cha pace maker kwani mapigo yake ya moyo hayakuwa yanakwenda kama inavyotakiwa.
 
“Kwa mara ya kwanza niliwekewa kifaa hicho nchini India lakini hivi karibuni nilifanyiwa tena upasuaji baada ya kile cha awali kuishiwa nguvu na hivyo nikabadilishiwa kingine hapa JKCI. Na afya yangu inazidi kuimarika kama unavyoniona,” anasema. 
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2016/05/25/160525143227_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_3_640x360_bbc.jpg Rais Dk. John Magufuli akifurahia jambo na Profesa Janabi

Masharti magumu

Anasema mtu yeyote anayeugua magonjwa ya moyo anatakiwa kuwa makini na
mwenendo wa afya yake.
 
“Baada ya kuwekewa pace maker nilishauriwa kuwa mwangalifu katika ulaji wangu, hivyo huwa napendelea kula vyakula vya kuchemsha, nikienda kwenye sherehe mbalimbali huwa najiepusha kula vyakula kama vile wali, pilau.
 
“Huwa napendelea kula mbogamboga za majani kwa wingi mfano ‘caul flower’ hii mboga inafanana na kabeji, nakula maharage, samaki wa kuchemsha, ndizi, sukuma wiki, na matembele, matunda kama vile tikiti maji, apple, machingwa, mananasi, papai, haya matunda hutegemeana na msimu ulipo,” anasema.
 
Anasema hata hivyo huwa anapendelea zaidi kubeba juisi aliyoitengeneza kutoka nyumbani kwake na kwamba huepuka zile zinazouzwa madukani.
 
“Huwa nalazimika kupima uzito wangu kila mara, kuhakikisha kwamba hauzidi ule nilioshauriwa na daktari. Siruhusiwi kuzidi kilo 71, daktari wangu hunitaka niwe ‘flexible’,” anasema.
http://www.ippmedia.com/sites/default/files/articles/2016/08/12/Jengo%20la%20Taasisi%20ya%20Moyo%20Jakaya%20Kikwete%20lililopo%20katika%20Hospitali%20ya%20Taifa%20Muhimbili%20jijini%20Dar%20es%20Salaam..JPG Anasema jambo lingine analotakiwa kulizingatia ni matumizi ya dawa anazopaswa kuzitumia kila siku.
 
“Moyo wangu ulikuwa unatanuka, kitalamu tatizo hilo wanaliita ‘idiopathic vardiomyomyo pathy’. Baada ya kuwekewa kifaa hiki,
nimeendelea kufundisha kama kawaida,” anasema.
 
Aanguka ghafla 

Profesa huyo anasema jambo ambalo hatalisahau ni pale alipoanguka siku
moja wakati alipomaliza kupandisha ngazi kuelekea darasani kufundisha.
 
“Siku hiyo nakumbuka nilikuwa nimepandisha ngazi haraka haraka, nilipata shork, nikaanguka, wanafunzi wangu walikuja na kunisaidia kuniinua pale chini, nikawaambia wasiogope kwani nikipumzika kidogo nitakuwa vizuri.
 
“Kweli waliniacha nikampuzika nikarejea katika hali yangu ya kawaida na nikaendelea kufundisha. Kila siku huwa natumia dakika 45 kufundisha, na wakati mwingine huwa zinazidi,” anasema.
 
Marufuku kuweka simu upande wa moyo 

Anasema hili ni miongoni mwa masharti ambayo watu wanaofanyiwa upasuaji wa kuwekewa pace maker hutakiwa kulizingatia.
 
“Siruhusiwi kuweka simu au kitu chochote chenye sumaku upande wa kushoto ambapo ndipo moyo ulipo. Aidha siruhusiwi kupiga simu upande wa kushoto au tablet,” anasema.
https://bloggerimports.files.wordpress.com/2008/11/moi3.jpg Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akimjulia hali mmoja wa watoto waliofanyiwa upasuaji.

Anasema kila siku hutakiwa kunywa maji kiasi cha lita moja na nusu, lakini kwa upande wa komputa hakuna tatizo hivyo huwa inakaa mbele yangu kama kawaida,” anasema. 

Anasema pia haruhusiwi kubeba kitu chochote chenye uzito.
 
“Nashukuru Mungu hadi majirani zangu wanajua hali yangu niliyonayo, zamani hata mlango ukibamizwa nilikuwa napata shida lakini sasa nimezoea naona kawaida,” anasema.
 
Moyo hupaswa kupiga mara 70
 
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi anasema kwa kawaida kwenye moyo kuna ‘system’ imekaa kama umeme na hiyo ndiyo inayosafirisha mawasiliano ili moyo uwee kupiga na kupumzika.
 
“Kwa kawaida tunachotegemea moyo lazima upige mara 70 kwa dakika na utoe damu mililita 70, hivyo 70 mara 70 ni 490 ambazo ni sawa na lita tano na hiyo ndiyo dmu yetu kwa kawaida.
 
“ule mfumo ukibadilika mapigo ya mtu hupiga chini ya kiwango hicho na ndipo hapo unakuta wengi huzimia na kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku za kijamii na kiuchumi,” anasema.
 
Anasema wapo ambao hupoteza fahamu kati ya mara tano hadi sita kwa siku. 

Gharama ya pacemaker ni kubwa.
 
Anasema ili kuwekwa kifaa hicho nchini India hugharimu hadi Dola 25,000 sawa na milioni 20 kwa mtu mmoja hiyo ni bila kujumuisha
gharama za usafiri, chakula na malazi.


“Ni ghali kuweka pace maker, sasa wagonjwa wetu baadhi yao walikuwa na bima ya afya, hapa JKCI tunaweka kwa Sh milioni 8.5 kwa wale wasiokuwa na bima hadi milioni 40.
 
"Hivyo nawasihi watu kukata bima kwani ni lazima vifaa hivi vinunuliwe na vinapatikana nje ya nchi kwa gharama kubwa,” anasema. 

Idadi ya waliofanyiwa upasuaji 

Profesa Janabi anasema tangu mwaka 2013 hadi sasa tayari wamefanya 'procedure' 562 katika mtambo maalumu (cath lab).
https://scontent.cdninstagram.com/hphotos-xaf1/t51.2885-15/s320x320/e35/12142548_115104575515754_1846199046_n.jpg "JKCI tunaweka pia vyuma kwenye mishipa iliyoziba, mwaka huu pekee wagonjwa zaidi 45 tumeshawawekea na wanaendelea vizuri.
 
"Tayari tumefanya upasuaji mkubwa wa kutibu moyo kwa kufungua kifua kwa watu 326. 

"Upasuaji unafaywa kwa uangalifu mkubwa hadi sasa vifo vilivyotokea ni vinane tu, " anasema. 

Moyo ni nini
 
Hii ni ogani ya mwili inayoendesha mzunguko wa damu mwilini. Kazi yake kuu ni kusukuma damu kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgb_roMeMg7Q00sklVuPzGgLO1GbHU0l_Hv8I0fSedH6h7HaJGz7B5DplZr5BHRT5AnrCmjaSXii6PEtpb_WWsRyF4PZPnLi7hQEUYCLimyT8oBTjBusWJyyfgqUGvTFkWm7tfC5iRwXFc/s1600/WAZIRI-UMMY.jpg Kikundi cha Baps Charity kikikabidhi msaada wa fedha kusaidia matibabu ya watoto kwenye taasisi hiyo, hivi karibuni

Kwa kawaida moyo wa viumbe walio katika kundi la mamalia ikiwa ni pamoja na binadamu huwa una pande mbili.
 
Upande wa kulia huwa unasukuma damu kwenda mapafu inapopokea oksijeni, upande wa kushoto unazungusha damu katika sehemu nyingine za mwili pale ambako oksijeni iliyopokelewa huhitajika.
 
Inaelezwa kwamba moyo ni ogani ya lazima kwa uhai. Mishipa ya damu moyoni huwa na majina maalumu.
 
Kwa jumla kuna mishipa mikubwa kwa sababu damu yote inapaswa kupita humo.
 
Kwa hiyo mishipa karibu na moyo ni kama barabara kuu za damu mwilini.
 
Mishipa yote inayopeleka damu kwenda moyoni huitwa vena.
 
Aidha mishipa yote inayotoa damu kutoka kwa moyo kwenda sehemu nyingine za mwili huitwa ateri.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7hJG_3P_yqxhHtHrY6U1LlHsBu1Zxb-fsBWKTlUY_FKW1If04PAvLc8pl8K8pgvp5IyBQ1akGrh7ovSIqaogXnX2t3tlcsm8L1Xinhv6KeqD6waqxKfOSn8TB31bU1gsT62_EE8onFyXX/s1600/DSC_0704.JPG Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi hivi karibuni alipotembelea taasisi hiyo.


Ateri kuu inayopeleka damu mwilini inaitwa aorta. Zipo pia ateri za nje zinazozunguka moyo mwenyewe.
 
Ikiwa misuli inahitaji oksijeni kwa kazi yake. Ateri za nje zinafikisha damu yenye oksijeni moja kwa moja kwa seli za moyo wenyewe.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement