Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
https://www.cdc.gov/reproductivehealth/images/maternal-infant-health/tobacco/tobacco-use-pregnancy-woman-carrying-250px.jpg 

Na Sweetbert Hudson - SAUT

Jumla ya kinamama wajawazito 35 wamefamyiwa uchunguzi wa kipimo cha magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga waliopo tumboni mwa mama zao (FETAL ECHOCARDIOGRAPHY) ili kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la.

Majibu ya kipimo hicho yalionyesha kuwa kati ya hao watoto watano walikutwa na matatizo ya moyo jambo ambalo litawawezesha   kupata matibabu mapema pindi watakapozaliwa.

Hayo yamesemwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani wakati akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.

Dkt. Naiz alisema kipimo hicho hakina madhara yoyote kwa mama na mtoto na kina  uwezo wa kugundua endapo mtoto ameathirika na ugonjwa wa moyo na hivyo kumuandaa mama mjamzito kwaajili ya uzazi salama.

“Mojawapo ya dalili za mama mjamzito ambazo zinaweza pelekea kupata mtoto mwenye  tatizo la ugonjwa wa moyo ni pamoja na ugonjwa wa kisukari,shinikizo la damu,matumizi ya dawa za muda mrefu,mimba ya mapacha, kuwepo na mtu mwenye tatizo la moyo katika familia na mimba pandikizi”. 

“Ninawaomba kina mama wajawazito wenye moja ya dalili nilizozitaja waje tuwafanyie kipimo hiki  kipindi  ambacho mimba zao zitakuwa na umri wa kati ya miezi minne hadi saba hii itawasaidia  kugundua afya za watoto wao na kuepuka na vifo vya mara  baada ya kuzaliwa vinavyotokea kipindi cha mwezi mmoja hadi mwaka”, alisema Dkt. Naiz.

Alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa kinamama wajawazito juu ya kipimo hicho kwa kufikiria kuwa kinamadhara  jambo ambalo siyo kweli kwani kipimo hicho hakina  madhara yoyote kiafya.

Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete (JKCI) ilianza kutoa huduma hiyo tangu mwezi wa tatu mwaka huu ili kupunguza  vifo vya watoto vinavyotokana na  magonjwa ya moyo mara baada ya mtoto kuzaliwa.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement