Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akikagua moja kati ya Friji ya kuhifadhia chanjo.
WAMJW-KATAVI
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi kutumia
nguvu kazi yao katika ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao
kuliko kupeleka pesa nyingi kwa wakandarasi.
Dkt.Ndugulile ameyasema hao wilayani
hapa wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za utoaji huduma za
afya na kutathimini shughuli za maendeleo ikiwemo ya upanuzi wa
miundombinu zikiwemo ya Zahanati.
Alisema kutumia nguvu kazi zao
itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza
kama wangetoa tenda hiyo kwa wakandarasi.
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akiwaonesha nembo ya MSD GOT inayotambulisha kuwa Dawa hiyo inatolewa na
Serikali kwa wananchi.
“Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa
shughuli hizi na mkiharibu tutakuja kuwalaumu nyinyi,” alisema.
Aidha,alisema Serikali imetoa
shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya huduma za
afya nchini kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi
ya wazazi,maabara ,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya
afya ambapo ujenzi huo unaanza mara moja.
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa
ndani ya duka la Dawa la MSD kufanya ukaguzi juu ya upatikanaji wa Dawa zote,
Kulia ni Mfamasia wa duka hilo Bahati Kazimili.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile
ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa, huku
akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu kwani hali ya upatikanaji
wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.
“Katika kituo cha Afya Kanoge, bajeti
ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo
za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa aambiwe akanunue dawa sehemu
nyingine, wamenithibitishia waganga wangu asilimia 90 ya dawa muhimu zipo”
aliendelea Dkt. Ndugulile
Wakati huo huo Dkt. Ndugulile
amesisitiza watumishi wa afya juu ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa katika stoo
ya madawa ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa zilizoingia na kutoka pamoja na
utunzaji wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa kila siku, jambo linalopunguza
ufanisi katika kazi.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge kuanzisha ofisi ya kushughulikia
malalamiko ya watu pindi wanapokutana na changamoto wakati wakipata huduma
katika Kituo hicho cha Afya.
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akikagua mashine ya Utla Sound wakati
akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma
za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi wenyewe
kwa kushirikiana na Serikali.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dkt. Yahaya Hussein wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa alisema kuwa Mkoa
wa Katavi unakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya hali
inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hadi kufikia Septemba 2017 Mkoa wa
Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na asilimia 28 kati ya watumishi 2,437
wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya
Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una jumla ya upungufu wa watumishi
1,744” Alisema Dkt. Hussein.
Dkt. Yahaya Hussein aliongeza
kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa
ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee ili kuendelea kupata
Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.
Mpaka kufikia Mwezi Septemba 2017
jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao jumla ya wazee 1,807 sawa
na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika Halmashauri zote za Mkoa wa
Katavi.
Chapisha Maoni