Jumatano, 3 Januari 2018

WASIOFANYA VEMA TENDO LA NDOA HATARINI KUPATA TEZIDUME - UTAFITI

Picha na mtandao

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mwanaume anayeshiriki vema tendo la ndoa kwa kiwango kinachostahili hujiepusha kupata saratani ya tezidume kuliko yule ambaye hufanya kwa kiwango kisichostahili.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Ocean Road, Mark Mseti alisema hayo alipozungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu.

Alisema zipo tafiti ndogondogo ambazo zimewahi kufanyika duniani zinazothibitisha ukweli juu ya jambo hilo.

“Hazijawahi kufanyika tafiti kubwa, lakini inaelezwa angalau mwanume aliyekamilika anapaswa kushiriki angalau mara tatu kwa wiki ingawa wapo pia ambao hujiweza na kuvuka zaidi ya hapo,” alisema.

Aliongeza “Hii haimaanishi kuwa mzinzi… ukiwa mzinzi maana yake utapata magonjwa mbalimbali hasa ya zinaa na hivyo kujiweka kwenye hatari zaidi.

Hapa nimekuwekea kwa kifupi, habari hii imetoka leo kwa kina kwenye gazeti la MTANZANIA, hivi karibuni usikose nakala yako alhamis ambapo utasoma kwa undani makala ya mahojiano na Dk, Mseti ameeleza kwa kina kuhusu tatizo hilo, visababishi vingine, dalili na matibabu yake.