Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi, (wa pili kushoto), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Peter Kissenge na Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Samiro Pharmacetical, Masila Mani.g wakiwa katika picha ya pamoja na Mfanyakazi bora wa mwaka 2017 JKCI, Muuguzi Mkuu Mwandamizi wa JKCI, Hadija Mnadi.
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI), Profesa Mohamed Janabi amewatunuku vyeti na zawadi wafanyakazi bora wa
mwaka 2017.
Hafla hiyo imefanyika mapema leo katika ukumbi wa mikutano
wa Taasisi hiyo, vyeti na zawadi hizo zimetolewa na Kampuni ya Samiro
Pharmacetical.
Akizungumza, Prof. Janabi amesema hatua hiyo imelenga kuwapa
motisha wafanyakazi wake ili wazidi kufanya kazi vyema zaidi katika kuhudumia
wagonjwa wanaowapokea.
“Taasisi yetu inafanya uchunguzi na kutoa matibabu kwa watu
ambao wanakabiliwa na magonjwa ya moyo, tunatoa huduma bora na ndiyo maana
tunaona tuwape motisha wafanyakazi wetu ili wazidi kufanya kazi kwa bidii na
tuzidi kutoa huduma bora zaidi,” amesema.
Aliwataja wafanyakazi waliotunukiwa vyeti na zawadi ni
Daktari Bingwa wa Watoto, Stella Mongella, Ofisa Mtunza Kumbukumbu za Utabibu
(THR II), Maimuna Hemed, Daaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Aloyce Mohamed na
Nesi Mkuu Mwandamizi Hadija Mradi.
Sambamba na hilo, Profesa Janabi amesema wamepanga kuanza kuwakopesha wafanyakazi wake mikopo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Janabi akimtunuku cheti Daktari Bingwa wa Watoto, Stella Mongella wakati wa hafla hiyo.Sambamba na hilo, Profesa Janabi amesema wamepanga kuanza kuwakopesha wafanyakazi wake mikopo mbalimbali.
“Tunataka tuwakopeshe wenyewe humu ndani kwa sababu kwenye taasisi zingine unakuta wanaweka riba kubwa, tukiwakopesha itawasaidia mno kiuchumi,” amesema.
Naye, Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Samiro Pharmacetical, Masila Mani.g amesema kampuni yao imekuwa na utaratibu wa kuwezesha vyeti na zawadi hizo kwa muda mrefu sasa katika taasisi hiyo.
“Si mara yetu ya kwanza, tunafanya hivi kwa sababu tunawajibika pia kurejesha kwa jamii na hatua hii inasaidia kuwapa motisha wafanyakazi hawa ili wazidi kutoa huduma bora kwa jamii,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Watoto, Stella Mongella na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Peter Kissenge na Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Samiro Pharmacetical, Masila Mani.g.
Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi akimtunuku cheti na zawadi, Ofisa Mtunza Kumbukumbu za Utabibu (THR II), Maimuna Hemed.
Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi akimtunuku, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Aloyce Mohamed wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi akizungumza na wafanyakazi wakati wa hafla hiyo.
Chapisha Maoni